Banda la Wizara ya Fedha ndani ya Nane Nane Dodoma

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Idara ya Kuondoa Umaskini, William Ghumbi (KUSHOTO) akiwaelimisha wananchi juu ya MKUKUTA II walipotembelea banda la Wizara ya Fedha mjini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane. Picha na HAZINA, Dodoma (Maria)

Ofisa kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania(UTT) Mvumo Balati (kushoto) akiwaelimisha Polisi faida kuwekeza katika mfuko huo leo mjini Dodoma wakati walitembelea maonyesho ya nanenane mjini Dodoma kwenye banda la Wizara ya Fedha.

Ofisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (kushoto) akiwahudumia maofisa Polisi walipotaka kujua kiwango cha michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma.

Mtunzaji Kumbukumbu na Mhasibu Abbas Mnyeto wa Wizara ya Fedha wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu jana mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma