Banda la Viwanda na Biashara lavuta wengi Nanenane Dodoma

Kaimu Kurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara, Ismael Mfinanga na Mkaguzi wa ndani wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Asia Mohamedi, wakipata maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Vicent Kone akipata maelezo ya bidhaa mbalimbali za mjasiriamali anayewezeshwa na Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonesho ya Nanenane mjini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Vicent Kone akipokelewa na maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara alipotembelea banda la Wizara hiyo katika Viuwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajasiriamali kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakishiriki mafunzo yanayotolewa na taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Viwanmda na Biashara ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa tija. Mafunzo hayo hutolewa bure kila siku asubuhi kabla ya kuanza kwa maonesho.

Maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika Banda la Wizara hiyo katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma tayari kwa kutoa huduma kwa wageni watakaotembelea banda hilo.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (Kushoto), akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) waliopo katika maonesho ya Nanenane mjini Dodoma. Picha zote na Kitengo cha Habari, Wizara ya Viwanda na Biashara