Balozi wa Vietnam Azungumza na Dk Asha-Rose Migiro

Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyen Duy Thien (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo, Januari 23, 2013, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) akizungumza na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyen Duy Thien, katika Ofisini Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 23, 2013. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela ambaye alijumuka katika mazungumzo hayo. Wengine ni Maofisa wa Makao Makuu ya CCM.