MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Iddi ametoa changamoto kwa wafanyabiashara na wazalishaji bidhaa wa hapa nchini kujifunza kuzalisha bidhaa zenye ubora kutoka kwa wafanyabiashara wa China na kuacha kuingiza bidhaa bandia au zisizobora.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu huyo wa Rais wakati akifungua maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini DaresSalaam.
“Monesho ya mwaka huu yatakwenda pamoja na maonesho ya bidhaa za China, ukiwa ni mkakati wa serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kudhiirisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini China.
“Lengoni kuwaonesha wafanyabiashara wetu kuwa China inao uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa bora na hivyo waanche kuingiza bidha bandaia au zenye ubora wa chini,”alisema Balozi Seif.
Aliongeza kuwa bidhaa hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya viwanda vya ndani na pi ushindani wa haki, kibiashara.
Balozi Seif alisema nchi ya China kwa sasa ni taifa la pili kwa nguvu za kiuchumi duniani, wanayo teknolojia ya hali ya juu ya kuzalisha bidhaa bora zinazouzwa duniani kote.
Alisisitiza kuwa Tanzania imepewa fursa ya kuuza bidhaa zaidi ya 400 nchini China bila ya viwazo vya kodi ya forodha wala ukomo wa kiasia cha mauzo.
Makamu huyo wa Rais alisema nchi za Kenya na Rwanda zimeshiriki katika maonesho hayo . Aliongeza kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimetoa fursa kwa nchi uancham kufanyabiashara kwa ushindani zaidi .
Hivyo aliwataka wanayabiasahra wa hapa nchini kutoa fusa za masoko hayo ili kuzalisha bidhaa bora na za kutosha.
Aidha Makamu huyo wa Rais aliongeza kuwa takwimu za biashara zinaonesa kuwa Tanzania ina urari chanya katika nchi za EAC lakini inaurai hasi kwa nchi nyingine kama jumuiya ya Ulaya na Asia.
“ Hii inatukumbusha umuhimu wa kuongeza uzalishaji na mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi. Ni muhimu pia kusindika bidhaa zetu kabla ya kuziuza nje,” alisisitiza.
Alisema usindikaji wa bidhaa una manufaa mengi ikiwemo kupta bei nzuri, kuongeza muda wa bidhaa huska kuwapatia ajira vijana na wanawake na kuendelea teknolojia katika nchi yetu.
Kauli mbinu ya maonesha hayo ni ‘Tanua Wigo wa Biashara Yako’.