Balozi Seif Ally akabidhi vifaa vya Zahanati Kimara

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni, Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakijimwaya mwaya kucheza muziki wa taarab, kushangilia makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba kwa Zahanati yao.