
Balozi wa Tanzania Nchini China, Philip Marmo akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China, baada ya kuwasili Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza, nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Beijing, China, Philip Marmo (wapili kushoto), baada ya kuwasili Machi 17, 2013 akitokea Sichuan. Kinana na Ujumbe wa viongozi 14 wa CCM yupo nchini China tangu Machi 11, mwaka huu, akiwa katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai na Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mjumbe wa Kamti Kuu ya CCM, Kadija Aboud.