Mchezaji Gareth Bale alifunga mabao matatu na kumfanya kocha mpya wa kilabu ya Real Madrid Zinedine Zidane kupata ushindi wa kwanza katika kazi yake dhidi ya Deportivo La Coruna mwishoni mwa wiki.
Karim Benzema alifunga bao lake la 100 katika ligi ya Uhispania alipoiweka timu yake kifua mbele katika dakika za kwanza tangu kuondoka kwa aliyekuwa mkufunzi Rafael Benitez.
Bale alifunga bao la pili ,la tatu na la nne na hivyobasi kufunga udhia wa mabao yake matatu na Benzema alifunga bao la tano na kuiweka Real Madrid alama mbili nyuma ya viongozi Barcelona.
Naye Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Barcelona kupata ushindi wa rahisi dhidi ya Granada na kurudi kileleni mwa ligi ya La Liga.
Raia huyo wa Argentina alifunga mara mbili katika dakika 15 za kwanza na kuongeza bao jingine baada ya mda wa mapumziko hivyobasi kuongeza idadi ya mabao aliyofunga kufikia 18 huku Barcelona ikifaulu kucheza mechi 20 bila kupoteza.
Messi aliiweka Barcelona kifua mbele baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji matata wa timu hiyo Louis Suarez, Aliongeza bao la pili katika dakika ya 58 kabla ya Neimar kufunga bao la nne.