JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHE. SAADA MKUYA SALUM (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA MWAKA 2015/16 Dodoma JUNI, 2015
1
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa
Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi,
Viwanda na Biashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu
sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2015/16.
2. Mheshimiwa Spika, Awali ya yote namshukuru
Mwenyezimungu, mwingi wa rehma kwa kuniwezesha kusimama
mbele ya Bunge lako Tukufu nikiwa na afya njema ili kushiriki
mkutano huu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapongeza kwa dhati
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao mahiri
uliyoiwezesha nchi yetu kufanya vema katika nyanja ya uchumi.
4. Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa pongezi zangu za dhati
kwa Bunge lako Tukufu kwa kazi nzuri ambayo limeifanya katika
kipindi chote cha uongozi wako. Nakupongeza wewe binafsi, kwa
kuliongoza Bunge letu tukufu kwa busara za hali ya juu katika
kutimiza majukumu yake.
5. Mheshimiwa Spika, naomba pia niwashukuru Naibu Mawaziri
wa Wizara ya Fedha, Mheshimiwa Adam Kighoma Ali Malima (Mb) na
Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa ushirikiano mkubwa
wanaoendelea kunipa katika kutekeleza majukumu yangu na pia kwa
mchango wao mkubwa katika maandalizi ya bajeti hii. Namshukuru
Katibu Mkuu Dkt. Servacius B. Likwelile, na Naibu Makatibu Wakuu
Prof. Adolf F. Mkenda, Bibi Dorothy S. Mwanyika na Dkt. Hamis H.
Mwinyimvua kwa kazi nzuri wanayoifanya. Aidha, ninapenda
kuwashukuru Prof. Benno Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
na Bw. Rished Bade, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania. Aidha, nawashukuru Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu
wa Taasisi, Wakuu wa Vitengo na wafanyakazi wote wa Wizara ya
Fedha na Taasisi zake kwa kazi nzuri na ushirikiano wao mkubwa.
Ninawaomba wadumishe ushirikiano wanaonipa ili wizara iendelee
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
6. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru
wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge wote, kwa
kuendesha majadiliano ya bajeti ya mwaka 2015/16 kwa umakini
tangu yalipoanza hadi sasa. Aidha, nawashukuru kwa namna ya pekee
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na
Biashara, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Joelson Luhaga
Mpina, Mbunge wa Kisesa kwa maoni, ushauri na mapendekezo
waliyoyatoa. Wizara imezingatia ushauri na mapendekezo ya Kamati
katika kukamilisha uandaaji wa hotuba hii.
7. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii pia
kuwapongeza Mhe. Dkt Grace Pujah (Mb) na Mhe. Dkt Innocent Seba
(Mb) kwa kuteuliwa kwao na Mheshimiwa Rais kuwa wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
8. Mheshimiwa Spika, naungana na Waheshimiwa Wabunge
wenzangu kutoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wananchi kwa
kifo cha Mheshimiwa Kapt. John Damiano Komba, aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la Mbinga Magharibi. Aidha, natoa pole kwa wananchi wote
kwa ujumla kutokana na matukio ya ajali barabarani na maafa
yaliyotokana na mafuriko makubwa yaliyotokea sehemu mbalimbali
nchini. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema
peponi, Amina.
MAJUKUMU YA WIZARA
9. Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara ni pamoja na kubuni
na kusimamia utekelezaji wa sera za uchumi jumla, kusimamia
ukusanyaji wa mapato ya ndani na ya nje pamoja na matumizi ya
Serikali; kuandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali;
kufuatilia utekelezaji wa mipango ya kupunguza umaskini katika sekta
mbalimbali; kusimamia Deni la Taifa; kusimamia upatikanaji wa
rasilimali fedha zinazotumika katika miradi ya ubia kati ya Serikali na
sekta binafsi; kusimamia sera, sheria, kanuni na taratibu za uhasibu,
ukaguzi wa ndani na ununuzi wa umma; kusimamia mali ya Serikali;
kusimamia taasisi na mashirika ya umma; kusimamia masuala ya
Tume ya Pamoja ya Fedha; kuandaa na kulipa mishahara ya
watumishi wa Serikali; kusimamia ulipaji wa mafao na pensheni ya
wastaafu; na kudhibiti biashara ya fedha haramu pamoja na ufadhili
wa ugaidi.
4
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA
KWA MWAKA 2014/15 NA MALENGO YA MWAKA 2015/16
10. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, majukumu ya
Wizara yaliendelea kutekelezwa kupitia mafungu saba ya kibajeti.
Mafungu hayo ni Fungu 50 – Wizara ya Fedha; Fungu 21 – Hazina;
Fungu 22 – Deni la Taifa; Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa
Serikali; Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha; Fungu 13 – Kitengo
cha Udhibiti wa Fedha Haramu; na Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa
Hazina. Aidha, utekelezaji wa Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
umejumuishwa katika hotuba hii kwa kuwa fungu hili huombewa
fedha na Waziri wa Fedha.
11. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka
2014/15 umezingatia malengo ya Mpango Mkakati wa Wizara; Mpango
wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12 – 2015/16; Mkakati wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA);
Malengo ya Maendeleo ya Milenia, 2015; Mkakati wa Pamoja wa
Misaada Tanzania (MPAMITA) pamoja na Programu ya Maboresho ya
Usimamizi wa Fedha za Umma. Vile vile, Mpango na Bajeti umezingatia
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 pamoja na
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
12. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, pamoja na mambo
mengine, Wizara ilipanga kutekeleza yafuatayo:
i. Kusimamia sera za mapato na matumizi ya fedha za Serikali;
ii. Kusimamia udhibiti wa matumizi ya fedha za umma;
iii. Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Awamu ya Nne ya
Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma;
iv. Kukamilisha Sera ya Taifa ya Mali ya Umma;
v. Kusimamia Ununuzi wa Umma;
vi. Kuimarisha usimamizi wa mashirika na taasisi za umma;
vii. Kufanya mapitio ya utekelezaji wa MKUKUTA II;
viii. Kuendelea kuboresha huduma za pensheni kwa wastaafu na
malipo ya mirathi;
ix. Kuandaa miongozo mbalimbali ya ukaguzi wa ndani;
x. Kufanikisha upatikanaji wa fedha za misaada na mikopo nafuu
na ya kibiashara;
xi. Kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo ya maafisa ununuzi na
ugavi kwenye wizara, idara na taasisi zinazojitegemea nchini;
xii. Kukamilisha stadi ya kubainisha mwenendo wa uchumi na
mapato ya muungano wa Tanzania;
xiii. Kuendelea kulipa madeni ya ndani na nje kwa wakati;
xiv. Kusimamia, kuimarisha na kuboresha uendeshaji na
uunganishaji wa mtandao wa malipo ya Serikali; na
xv. Kuendelea kupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku
zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi;
13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imetekeleza
majukumu yake kama ifuatavyo:-
Mwenendo wa Ukusanyaji wa Mapato
(a) Mapato ya Ndani
6
14. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, sera za mapato
zililenga kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi
bilioni 12,638.5 (ikijumuisha mapato ya mamlaka za serikali za mitaa).
Hadi Aprili 2015, jumla ya makusanyo ya ndani (ikijumuisha mapato
ya mamlaka za serikali za mitaa) yalikuwa shilingi bilioni 8,924.9,
sawa na asilimia 71 ya makadirio.
15. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha ukusanyaji wa kodi, Wizara
imeendelea kupitia sheria na taratibu mbalimbali kwa minajili ya
kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na kupanua wigo wa kodi. Katika
jitihada hizi, Wizara imefanikisha kupitisha Sheria ya Usimamizi wa
Kodi ya Mwaka 2014 na sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
ya Mwaka 2014.
16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo:- kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani
kwa kuchukua hatua mbalimbali katika maeneo ya mapato
yatokanayo na kodi na yasiyo ya kodi kwa kuanisha vyanzo vipya na
kupanua wigo wa kodi; kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na
kudhibiti upotevu wa mapato; kuchukua hatua za kudhibiti na
kupunguza misamaha ya kodi; na kuboresha mfumo wa ukusanyaji
wa kodi za majengo.
(b) Usimamizi wa Misaada na Mikopo
17. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikisimamia na
kuhakikisha ufanisi katika misaada tunayopokea kutoka kwa
Washirika wa Maendeleo. Katika kuboresha ushirikiano kati ya
Serikali na Washirika wa Maendeleo, Wizara imeandaa rasimu ya
Muongozo wa Ushirikiano yaani Development Cooperation Framework
(DCF) ambao rasimu ya mwisho imekamilika na ipo katika hatua za
kuidhinishwa na Serikali. Muongozo huu umezingatia maoni ya wadau
wote ikiwa ni pamoja na Wadau wa Maendeleo, Wabunge, Asasi za
Kiraia, Sekta Binafsi, Wanazuoni, na Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Aidha, muongozo huu una masuala muhimu katika ushirikiano wa
kimaendeleo ikiwemo namna ya kupokea fedha za maendeleo,
uwajibikaji, masuala ya majadiliano pamoja na kufanya tathmini na
ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
18. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Wizara itaandaa
Mpango kazi wa kutekeleza DCF ili kuboresha ushirikiano kati yake na
washirika wa maendeleo. Pia kufuatia kukamilika kwa DCF na
kuidhinishwa, Wizara itasambaza DCF kwa wadau ili iweze kutoa
muongozo wa ushirikiano. Ili kufanya muongozo huo kueleweka na
kutumika kwa urahisi, Wizara itatafsiri DCF kwa Lugha ya Kiswahili
pamoja na kuhakikisha eneo la Majadiliano linaboreshwa na kupatiwa
muongozo kama DCF ilivyoelekeza.
Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
19. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara imetekeleza
yafuatayo: kuratibu uandaaji wa Mwongozo wa Mpango na Bajeti kwa
kipindi cha 2015/16-2017/18 kwa wizara, idara zinazojitegemea,
taasisi na wakala wa Serikali, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa
na kusambaza kwa wadau; kuratibu vikao vya uchambuzi wa bajeti ya
mwaka 2015/16 kutoka wizara, idara zinazojitegemea, taasisi na
wakala wa Serikali, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa; na kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali, Wizara imeandaa na kusambaza
kwa wadau vitabu vya bajeti ya mwaka 2015/16 (Volume I, II, III & IV).
20. Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa ni
pamoja na: kuandaa, kuchapisha na kusambaza kitabu cha tafsiri
rahisi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2014/15 yaani “Citizen’s
Budget”; kutoa mafunzo juu ya kuandaa mipango na bajeti kwa
maafisa mipango, wahasibu na watakwimu 120 wanaoshiriki katika
uandaaji wa mipango na bajeti za mikoa na mamlaka za serikali za
mitaa; kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika
wizara 3, idara zinazojitegemea 2, mikoa 16, mamlaka za Serikali za
mitaa 49 na taasisi za Serikali 5 na kutoa mapendekezo ya kuboresha
mfumo wa udhibiti wa matumizi ya fedha za umma.
21. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kuboresha Mfumo
Mkakati wa Utayarishaji wa Mgawo wa Bajeti (Strategic Budget
Allocation System) ili kurahisisha uandaaji wa bajeti ya Serikali kama
ilivyoelekezwa katika Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti wa
mwaka 2014/15 – 2016/17. Vile vile, Wizara iliratibu vikao mbalimbali
na wadau wakiwamo Washirika wa Maendeleo kwa lengo la kutathmini
na kuboresha utekelezaji wa Bajeti ya Serikali.
22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara inatarajia
kutekeleza yafuatayo: kuandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya
Serikali inayojumuisha matumizi mengineyo, mishahara na
maendeleo; kupitia mfumo wa uwasilishaji wake na kuhakikisha kuwa
Sera na Mipango ya Kitaifa na ile ya Kisekta inazingatiwa ipasavyo;
kufanya tathmini ya Bajeti ya Serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa
inazingatia mahitaji ya makundi yote ya jamii; na kuimarisha mifumo
ya TEHAMA ya uandaaji bajeti ili kukidhi mahitaji ya taarifa
mbalimbali zinazohitajika.
23. Mheshimiwa Spika, Wizara pia itaendelea kuzijengea uwezo
wizara, idara za Serikali, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa katika
uandaaji wa bajeti ya muda wa kati, usimamiaji wake na utoaji taarifa
za utekelezaji ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathmini kwa wakati;
kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa bajeti ya Serikali ili
kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unazingatiwa; kufuatilia matumizi
ya fedha za umma zikiwemo fedha za mishahara, matumizi mengineyo
na fedha za Miradi; na kuimarisha uwezo wa Wizara katika kusimamia
utekelezaji wa bajeti ya Serikali.
Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma
24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara imeendelea
kuimarisha usimamizi wa fedha za umma kwa kutekeleza yafuatayo:
kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 357 wa kada ya
uhasibu, ugavi, na TEHAMA kutoka wizara, idara za Serikali,
sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa; kusimamia
ufungaji wa mfumo wa kielektroniki wa malipo ya kibenki – TISS na
kuanza kutumika katika Hazina Ndogo zote nchini; kuandaa hesabu
za majumuisho kwa kutumia viwango vya kimataifa – IPSAS Accruals;
kuhakiki wastaafu wote wanaolipwa pensheni kupitia Wizara ya
Fedha; kuratibu utayarishaji hesabu na taarifa za Wizara na Idara
zote za Serikali; na kusimamia uendeshaji mtandao wa malipo wa
Serikali kwa kutoa ushauri wa kitaalamu na kuziwezesha wizara,
idara za Serikali na mikoa kutumia mtandao kwa ufanisi.
25. Mheshimiwa Spika, hatua nyingine zilizochukuliwa kuimarisha
usimamizi wa fedha za umma ni kurekebisha sheria mbalimbali za
fedha kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2014. Aidha, Bunge lilipitisha
Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2014 na Sheria ya Mifumo ya Malipo Nchini
ya Mwaka 2015. Katika mwaka 2015/16, Wizara itakamilisha
muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana
za Serikali na marekebisho ya Sheria ya Msajili wa Hazina. Aidha,
Wizara itakamilisha maandalizi ya kuwezesha kutungwa kwa Sheria ya
Usimamizi wa Vituo vya Pamoja Mipakani.
26. Mheshimiwa Spika, ili kudhibiti matumizi ya fedha za umma
Wizara ya Fedha imeendelea kufanya ukaguzi wa ndani wa mara kwa
mara kwa wizara na taasisi za Serikali. Katika kutekeleza jukumu hilo,
Wizara ilifanya uhakiki wa madai mbalimbali ya watumishi wa
Serikali, watoa huduma na wakandarasi kabla ya kuyalipa. Wizara pia
imetayarisha Miongozo ya Usimamizi wa Vihatarishi, Udanganyifu,
Kuimarisha Mifumo ya Udhibiti wa Ndani, Ufuatiliaji na Tathmini ya
Usimamizi wa Vihatarishi, Ukaguzi wa Ununuzi, na Ukaguzi wa
Mikataba katika Sekta ya Umma. Miongozo hii itatumiwa na Wakaguzi
wa Ndani na wadau wengine katika sekta ya umma ili kuwajengea
uwezo na kuboresha utendaji kazi.
27. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya ukaguzi wa mfumo wa
malipo ya mishahara katika taasisi za Serikali; ukaguzi wa kiufundi
katika miradi 21 ya maji, barabara na majengo katika mikoa ya Lindi
na Mtwara na miradi 5 ya umwagiliaji iliyo chini ya Mpango wa
Matokeo Makubwa sasa katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa na
Katavi. Aidha, ukaguzi maalum wa Kituo cha Matibabu na Hospitali ya
Kufundishia ya Chuo Kikuu Dodoma na malipo ya Pensheni katika
Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali vilifanyika. Vile vile, Wizara
ilifanya ukaguzi wa miradi 32 ya maendeleo katika mikoa ya Kigoma,
Manyara, Dodoma, Mara, Mtwara na Dar es Salaam. Ushauri wa
kuboresha mifumo katika maeneo husika ulitolewa.
28. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imetoa mafunzo mbalimbali kwa
wakaguzi wa ndani 354 na Maafisa 835 kutoka taasisi za Serikali
kuhusu utumiaji wa mfumo wa uchambuzi wa kielektroniki (IDEA
Analytical software), ukaguzi wa kiufundi, Mwongozo wa Usimamizi wa
Vihatarishi katika Sekta ya Umma, na ukaguzi unaozingatia maeneo
yenye vihatarishi.
29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo: kuendelea kutoa udhamini wa masomo kwa
Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani, Wagavi na Wataalamu wa TEHAMA
kutoka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa; kusimamia, kuimarisha na
kuboresha uendeshaji na uunganishaji wa mtandao wa malipo wa
Serikali; kuendelea kusimamia na kuratibu uunganishwaji wa mifumo
ya TEHAMA ya kifedha ya Serikali; na kusimamia udhibiti wa
matumizi ya fedha za umma katika Wizara na Idara za Serikali kupitia
mtandao wa malipo wa Serikali.
30. Mheshimiwa Spika, Wizara imepanga pia kutekeleza yafuatayo:
kutathmini Mfumo wa Orodha ya Malipo ya Mishahara ya Watumishi
wa Umma; kufuatilia utekelezaji wa Miongozo ya Ukaguzi wa Bajeti na
Mishahara; kukagua mfumo wa kuandaa Bajeti; kufanya ukaguzi
maalum; kuchambua majibu ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali Kuu na kuziwasilisha Bungeni.
Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma
31. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara imeendelea
kuratibu utekelezaji wa Awamu ya Nne ya Programu ya Maboresho ya
Usimamizi wa Fedha za Umma. Programu hii imeendelea kuimarisha
usimamizi wa fedha za umma na inatekelezwa katika maeneo
yaliyobainika kuwa na changamoto katika usimamizi wa fedha za
umma kama ilivyobainishwa katika taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali. Pamoja na mambo mengine, utekelezaji
wa programu hii umechangia kuboresha utendaji katika ofisi na
wizara zifuatazo: Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi;Wizara ya Mali Asili na
Utalii; Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI; Mamlaka ya Udhibiti wa
Ununuzi wa Umma; na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.
32. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo: kuunganisha na kuhuisha mifumo ya kifedha ili
kurahisisha upatikanaji wa taarifa za fedha kwa wakati; kukamilisha
mapitio ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana za Serikali na
kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani wa Serikali za Mitaa na Serikali
Kuu juu ya ukaguzi wa mifumo ya fedha, usimamizi na ukaguzi wa
vihatarishi, ukaguzi wa bajeti na mishahara, ukaguzi wa miradi na
matumizi ya mifumo ya kifedha.
Ukaguzi wa Hesabu za Serikali
33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi imekagua mafungu yote 49 ya Wizara na Idara za Serikali,
hesabu za Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara, Hesabu za Halmashauri
zote 162 za Wilaya, Miji Manispaa na Majiji, Mashirika ya Umma 106,
Balozi zote 32 zilizoko nje ya nchi, na Wakala 33 za Serikali. Ripoti zote
za ukaguzi tayari zimewasilishwa kwa Mheshimiwa Rais na katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukaguzi katika
mashirika mengine yaliyobaki unaendelea na upo katika hatua
mbalimbali.
34. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
mkoani Dodoma umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 na muda
wowote jengo hili litaanza kazi. Kwa kuanzia jengo hili litakuwa na ofisi
nne ambazo ni Ofisi ya ukaguzi mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Ukaguzi ya
Bunge, Ofisi ya Ukaguzi TAMISEMI na Ofisi ya Ukaguzi kanda ya Kati.
35. Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yakayotekelezwa ni
pamoja na kushiriki kikamilifu katika jukumu la kukagua taasisi za
Umoja wa Mataifa ambapo ofisi inaingia mwaka wa nne kuwa katika
Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UN Board of Auditors);
kuboresha mfumo wa ukaguzi kwa kutumia teknolojia ya kompyuta;
kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ili kuimarisha uwezo wao katika
kutumia mfumo wa Team Mate na ili waweze kuendana na mabadiliko
ya teknolojia katika ukaguzi wa kisasa; na kuendelea na uunganishaji
wa ofisi za Ukaguzi zilizoko mikoani na makao makuu kwa kutumia
Wide Area Network. Kwa kuanzia Ofisi 12 tayari zimeunganishwa.
36. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka
2015/16 imepanga kutekeleza yafuatayo: kukagua mafungu yote ya
Wizara, Mikoa, Halmashauri, Idara zinazojitegemea na Mashirika ya
Umma; kuimarisha ukaguzi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na
yasiyo ya kodi; kuanza maandalizi ya kukagua sekta ya gesi, mafuta
na madini kwa kuwajengea uwezo wakaguzi; na kuondoa wakaguzi
katika majengo ya wakaguliwa katika wizara zote na katika mikoa yote
kwa kuwaweka katika majengo yanayokamilika au ofisi mbadala za
kupanga. Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wakaguzi wote
hawatakuwepo katika ofisi za wakaguliwa ifikapo mwishoni mwa
mwaka wa fedha 2015/16.
Usimamizi wa Mali ya Serikali
37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara
imekamilisha rasimu ya Sera ya Mali ya Umma; na uthamini wa mali
ya Serikali katika mikoa nane na wakala moja. Aidha, Wizara
iliendelea na zoezi la uthamini wa ardhi na majengo ya Serikali kwa
wizara, idara zinazojitegemea na wakala wa Serikali.
38. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea na zoezi la kuondosha
mali chakavu katika wizara na idara za Serikali. Jumla ya shilingi
bilioni 1.03 zilikusanywa kutokana na mauzo ya mali chakavu na
utoaji wa leseni za udalali. Aidha, Wizara ilikamilisha uchambuzi na
ufuatiliaji wa hasara zilizotokana na madawa na vifaa tiba kuisha
muda wake wa matumizi kabla ya kutumika na mali nyingine za
Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 10.15 na ufutaji wa hasara
hizo ulifanyika kwa Azimio la Bunge Na. 5/2014.
39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imepanga
kufanya yafuatayo: kukamilisha mkakati wa Sera ya Mali ya Umma;
kufanya uthamini wa mali katika taasisi sita za Serikali; kuondosha
mali chakavu, sinzia na zilizokwisha muda wake; na kuhakiki mali
katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali.
Ununuzi wa Umma
40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara imetekeleza
yafuatayo: kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma ya
Mwaka 2011 na Kanuni zake za Mwaka 2013 kwa taasisi za Umma 40
ambapo jumla ya watumishi 168 walihudhuria mafunzo hayo;
kufungua ofisi mbili Kanda ya Mashariki na Kanda ya Kati za Mamlaka
ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma; na kutoa mafunzo kwa asasi za
kiraia 25 kuhusu masuala ya ununuzi wa umma. Aidha, Wizara
imeendelea kuhuisha taarifa za maafisa Ununuzi na Ugavi katika
mikoa ya Arusha, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa,
na Pwani.
41. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea na maandalizi ya
kuanzisha mfumo wa ununuzi kwa njia ya kielekroniki (e-procurement
system), Wizara imetoa mafunzo kuhusu mfumo wa upokeaji na
usimamizi wa taarifa za ununuzi nchini katika vituo vya Mbeya,
Arusha, Morogoro na Mwanza ambapo jumla ya washiriki 368
walipatiwa mafunzo ya mfumo huo. Jumla ya taasisi 379 zimepatiwa
mafunzo na kuunganishwa kwenye mfumo huu, hii ikiwa ni sawa na
asilimia 84 ya taasisi zote.
42. Mheshimiwa Spika, katika usimamizi wa ununuzi kwenye Sekta
ya Umma, Wizara imefanya ukaguzi wa taratibu za utoaji wa zabuni
na utekelezaji wa mikataba itokanayo na ununuzi wa umma katika
jumla ya Taasisi 76 zikiwemo Wizara na Idara zinazojitegemea 17,
Mashirika ya Umma 16 na Serikali za Mitaa 43. Ukaguzi huu
umehusisha jumla ya Mikataba 4,532 yenye thamani ya shilingi bilioni
429.51. Maeneo yaliyobainika kuwa na upungufu ni katika usimamizi
wa mikataba na utunzaji wa nyaraka za zabuni.
43. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma ya ununuzi
Serikalini, Serikali imeanza utaratibu wa kununua magari kwa pamoja
kwa lengo la kupunguza gharama ambapo hadi Aprili, 2015 jumla ya
magari 179 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 10.197
yameagizwa. Hadi sasa mfumo huu wa ununuzi umeokoa kiasi cha
Dola za Marekani 989,514.17 kwa magari 50 ambayo yameshawasili.
Gari aina ya Toyota GX V8 ambalo lilikuwa linauzwa kwa bei ya Dola
za Marekani 122,726.8 lilinunuliwa kwa dola za kimarekani 75,591.32.
Gari aina ya Toyota Prado TX lilinunuliwa kwa Dola za Marekani
56,301.64 badala ya 77,754.84.
44. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Bodi ya Wataalam wa
Ununuzi na Ugavi ilisajili na kuratibu mienendo na maadili ya
wataalamu wa ununuzi na ugavi ambapo hadi Aprili, 2015 jumla ya
wataalamu waliosajiliwa walikuwa 3,418. Aidha, Bodi ilikamilisha
kuandaa mitaala mipya ya mafunzo ya taaluma itakayoanza
kufundishwa mwaka 2015/16.
45. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Rufaa za
Zabuni za Umma iliendelea kusikiliza rufaa ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa ndani ya siku 45 kwa mujibu
wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011. Hadi Aprili 2015,
jumla ya rufaa 21 zilisikilizwa na kutolewa maamuzi. Kati ya hizo,
rufaa tisa wazabuni walishinda, rufaa sita Serikali ilishinda, rufaa tatu
zilifutwa kutokana na kutokidhi matakwa ya kisheria na rufaa tatu
zilifutwa na walalamikaji wenyewe. Aidha, Mamlaka iliendesha semina
kwa mikoa 10 ili kupata mawazo ya wadau wa ununuzi juu ya mfumo
mzima wa uwasilishaji na ushughulikiaji wa rufaa. Mikoa hiyo ni
Mbeya, Iringa, Lindi, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro Arusha, Katavi,
Njombe na Manyara.
46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo: kukamilisha utekelezaji wa mpango kazi wa
usimamizi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011;
kuendelea kusimamia ununuzi katika sekta ya Umma; kuelimisha
wadau mbalimbali kuhusu sheria hiyo na Kanuni zake za Mwaka
2013; kuendelea na maandalizi ya kuanzisha mfumo wa ununuzi kwa
njia ya kielektroniki; kuendeleza kazi ya kufunga mfumo wa usimamizi
na udhibiti wa mafuta katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa,
Mbeya na Mwanza; na kuongeza uwezo wa Wakala wa kuhifadhi
mafuta katika vituo vya mikoa ya Iringa, Mbeya na Morogoro.
47. Mheshimiwa Spika, Wizara imepanga pia kutekeleza yafuatayo:
kufanya tathmini ya uthabiti wa mfumo wa ununuzi wa umma nchini;
kujenga uwezo wa Maafisa Ununuzi na Ugavi Serikalini; kutekeleza
mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma;
kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 na
Kanuni zake za Mwaka 2013; na kuendelea na zoezi la kuhakiki taarifa
za Maafisa Ununuzi na Ugavi waliopo Serikalini.
Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma
48. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015, Wizara kupitia
Ofisi ya Msajili wa Hazina imetekeleza yafuatayo: kuchambua bajeti za
mapato na matumizi kwa taasisi na mashirika 133 yanayopokea
ruzuku ya Serikali kwa lengo la kubaini taasisi na mashirika ambayo
yanaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku ya Serikali; kuchambua
Taarifa za Hesabu za Mashirika ya Umma 65 na kutoa mapendekezo
ya marekebisho stahiki kwa Bodi za Wakurugenzi na Wizara husika
kwa lengo la kuboresha utendaji wa taasisi hizo; na kufanya
uchambuzi wa Miongozo ya kiutendaji kwa taasisi na mashirika ya
umma na kupitia kanuni za fedha 24, miundo ya utumishi 19, kanuni
za utumishi nane, na mikataba ya hiari nane.
49. Mheshimiwa Spika, Vile vile, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa
Hazina imefanya kaguzi za Kimenejimenti katika Taasisi zifuatazo:
Rufiji Basin Development Authority (RUBADA); Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini – IRDP; Tropical Pesticides and Research Institute
(TPRI); na National Ranching Corporation (NARCO). Ushauri ulitolewa
kwa ajili ya kuboresha usimamizi katika Taasisi hizo. Aidha, Wizara
ilifanya uperembaji kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma 15
yaliyobinafsishwa kwa lengo la kukagua ufanisi na kuhakiki
utekelezaji wa masharti kulingana na Mikataba ya ununuzi. Mashirika
hayo yaliyobinafsishwa ni pamoja na Mwanza Textile, Shinyanga Meat,
Ilemela Fisheries, Manawa Ginneries, Blanket Manufacturing, Mtwara
Cashewnut Factory, Likombe Cashewnut, Newala I Cashewnut Factory,
Newala II Cashewnut Factory, Mtama Cashewnut Factory, Mufindi
Pyrethrum Factory, TTA Dabaga, Mufindi Tea Company, Ludodolelo
Pyrethrum Factory na Mahenye Farm.
50. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina
ilitoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuongeza mtaji wa Benki ya
Rasilimali – TIB; shilingi bilioni 50 – Kulipa Deni la PSPF (Pre-1999);
Nyongeza ya Mtaji wa Benki ya Kilimo shilingi milioni 500; Malipo ya
Pensheni kwa waliokuwa wafanyakazi wa Shirika la Simu – TTCL
shilingi bilioni 2 na Shirika la Posta – shilingi bilioni 1.74; TAZARA –
shilingi bilioni 4.33; na shilingi bilioni 1.97 zililipwa kwa PPF ikiwa ni
pensheni ya Wafanyakazi wa Vyuo vya Elimu ya Juu.
51. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Ofisi ya Msajili
wa Hazina itatekeleza yafuatayo: kuongeza ufanisi katika ukusanyaji
mapato yasiyo ya kodi kwa kuimarisha Mifumo ya upatikanaji taarifa
kutoka katika Taasisi kupitia TEHAMA, kuwajengea uwezo watumishi
katika maeneo ya uchambuzi wa kiufundi (Technical Analysis),
Tathmini ya Kazi (Job Evaluation), Uchambuzi wa Taarifa za Fedha
(Financial analysis), Uchambuzi wa Mikataba; kuendelea kuandaa
Mikataba ya Utendaji na Bodi za Wakurugenzi na Watendaji wakuu
kwa Mashirika na Taasisi zote, kufanya uhakiki wa Mali zilizoingizwa
katika Daftari la Mali ya Mashirika na Taasisi za Umma, kufuatilia na
kuhakiki mali zilizorithiwa kutoka Mashirika yaliyobinafsishwa ili
kuziingiza katika Daftari la mali ya Mashirika na Taasisi za Umma;
kufanya utafiti wa Taasisi zenye vyanzo binafsi vya mapato lengo likiwa
ni kuangalia uwezekano wa kuziondoa kwenye utegemezi wa ruzuku
ya Serikali.
Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara iliendelea
kushirikiana na wizara za ki-sekta katika kuendeleza progamu ya Ubia
Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP hapa nchini. Programu
hii imejumuisha kutoa mafunzo ya dhana ya Ubia kwa Taasisi za
Serikali ikwemo Mamlaka ya Bandari; Wakala wa Mabasi ya haraka –
DART; na Bohari Kuu. Aidha, Wizara imeendelea kutoa ushauri kwa
Wizara na Taasisi mbalimbali hususani katika utekelezaji wa miradi
iliyo chini ya Matokeo Makubwa Sasa – BRN. Vile vile, Wizara
imeshirikiana na wadau wengine kuandaa kanuni za sheria ya Ubia
iliyofanyiwa marekebisho mwezi Desemba 2014.
53. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 wizara imetenga
fedha katika Mfuko wa kuwezesha Miradi ya Ubia – PPP Facilitation
Fund – kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji
wanaochambua miradi ya Ubia na pia kuajiri Washauri – Elekezi
katika miradi ya Ubia. Tayari wizara imepokea maombi kutoka Taasisi
mbili za Serikali yaani TANROADS ili kugharamia Mshauri – Elekezi (
Transaction advisor) wa mradi wa Barabara ya Tozo ya Dar es Salaam
hadi Chalinze; na kutoka Bohari Kuu kwa ajili ya kugharamia Mshauri
– Elekezi wa mradi wa madawa muhimu. Wizara imeendelea
kuchambua maombi hayo ili kujiridhisha kiasi halisi cha fedha
zinazohitajika kabla ya kuziwasilisha kwa Taasisi hizo.
54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Wizara itaendelea
na jukumu lake la kisheria kuchambua miradi ya ubia
itakayowasilishwa na kituo cha Ubia Tanzania kwa lengo la
kuhakikisha kwamba miradi hii ina tija kwa Taifa; inakuwa endelevu;
na pia haiongezi deni la Taifa. Aidha, Wizara itaendelea kutoa ushauri
kwa wizara na Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kwamba
miradi bora inaibuliwa na kuendelezwa.
Uratibu wa Utekelezaji wa MKUKUTA
55. Mheshimiwa Spika, katika kuratibu utekelezaji wa MKUKUTA,
Wizara imetekeleza yafuatayo: kuandaa Taarifa ya Mwaka ya
Utekelezaji wa MKUKUTA II ya mwaka 2013/14; kuandaa Taarifa ya
Maendeleo ya Malengo ya Milenia ya mwaka 2014; na kuendelea na
utayarishaji wa Mfumo wa Taifa wa Kinga ya Jamii. Aidha, Wizara kwa
kushirikiana na Tume ya Mipango imeanzisha mapitio ya MKUKUTA II
na maandalizi ya mkakati mwingine. Vile vile, Wizara imeendelea
kushiriki katika majadiliano ya kimataifa ya kuandaa malengo ya
maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals 2030).
56. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuwafikia wajasiriamali
wadogo wadogo hasa vijijini, Mfuko wa SELF umeendelea kutoa
mikopo kwa wajasiriamali ambapo hadi kufikia Aprili 2015, mikopo
yenye thamani ya shilingi bilioni 5.74 ilikopeshwa kwa wajasiriamali
wadogo wadogo 2,834, kati yao 1,559 sawa na asilimia 55 ni
wanawake na wanaume ni 1,275 sawa na asilimia 45. Katika idadi hii
ya wajasiriamali vijana ni 856 sawa na asilimia 30. Aidha, kwa wastani
urejeshaji wa mikopo ya Mfuko wa SELF umeendelea kuwa wa ufanisi
katika kiwango cha asilimia 93 hivyo kuwezesha fedha za mfuko
kuzunguka na kuwafikia wajasiriamali wengi.
57. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2015/16 Wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo: kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali
kutoka katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali ili kuandaa taarifa
ya mwisho ya utekelezaji wa MKUKUTA; Kukamilisha Mfumo wa
ya Jamii ikiwa ni pamoja na kuandaa muundo wa viashiria vya
upimaji; na kuratibu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera za
kupambana na umaskini nchini. Aidha, Wizara kupitia Mfuko wa
SELF imepanga kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 18; na
kuendesha mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mikopo kwa
wajasiriamali 800 na wasimamizi 40 wa huduma za ushirika.
Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi
58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Wizara kupitia
Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu – FIU imepokea na kuchambua
jumla ya taarifa 98 zinazohusu miamala shuku ya fedha haramu na
ufadhili wa ugaidi. Aidha, taarifa 21 za kiintelijensia zimewasilishwa
kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na uchunguzi.
Aidha, ukaguzi umefanyika kwa watoa taarifa ambao ni benki 15,
kampuni za bima nne na Casino moja. Wizara pia imeandaa mwongozo
wa ukaguzi utakaotumika wakati wa kukagua watoa taarifa.
59. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha, kupitia Kitengo cha
Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) ilikagua benki za Stanbic na Mkombozi
kuhusu suala la ESCROW ACCOUNT. Taarifa ya kiintelijensia
iliyotokana na ukaguzi huo iliwasilishwa TAKUKURU kwa uchunguzi
zaidi. Hii ni kulingana na matakwa ya sheria ya kudhibiti utakasishaji
wa fedha haramu.
60. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ushirikiano katika
udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi na kubadilishana
taarifa za kiintelijensia na vitengo vya kudhibiti fedha haramu duniani,
Wizara ilijiunga na Umoja wa Vitengo vya Kudhibiti Fedha Haramu
Duniani. Aidha, Wizara imesaini Hati za Makubaliano na vitengo vya
kudhibiti fedha haramu vya Angola, Kenya, Zambia na Uganda na
hivyo kufikisha idadi ya hati nane za makubaliano na vitengo
mbalimbali. Wizara imeendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali
na vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria vya Tanzania Bara na
Zanzibar ambapo washiriki 99 walipata mafunzo.
61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara imepanga
kutekeleza yafuatayo: kuendelea kupokea na kuchambua taarifa za
miamala shuku zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili
wa ugaidi; kuwasilisha taarifa za kiintelijensia kwenye vyombo
vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi; kuratibu
zoezi la kutathmini mianya na viashiria vya fedha haramu na ufadhili
wa ugaidi nchini; na kutekeleza mikakati ya kitaifa na kimataifa ya
udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.
Tume ya Pamoja ya Fedha
62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia
Tume ya Pamoja ya Fedha imeendelea kufanya Stadi ya Uhusiano wa
Mwenendo wa Uchumi na Mapato ya Muungano ambayo lengo lake ni
kubaini mwenendo wa Mapato ya Muungano kutokana na ukuaji wa
uchumi; na kushauri njia bora ya kuimarisha Mapato hayo. Aidha,
Waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu mfumo bora wa uhusiano wa
kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT)
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) umeandaliwa na upo katika
hatua ya maamuzi. Maamuzi ya Serikali kuhusu waraka huu ndio
yatawezesha kufunguliwa kwa Akaunti ya Pamoja kati ya SMT na
SMZ. Vile vile, Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilisha mapendekezo
ya kufanya Stadi ya Uwekezaji Katika Mambo ya Muungano.
63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara kupitia
Tume ya Pamoja ya Fedha imepanga kukamilisha taarifa za stadi ya
uhusiano wa mwenendo wa uchumi na mapato ya Muungano na
kuiwasilisha katika pande mbili za Muungano. Aidha, Tume
inakusudia kuendelea kufanya stadi ya uwekezaji katika mambo ya
Muungano. Stadi hii inalenga kubaini ushiriki wa pande mbili za
Muungano katika uwekezaji kwa mambo ya Muungano.
Mpango wa Millenium Challenge Account- Tanzania
64. Mheshimiwa Spika, baada ya Serikali ya Tanzania kukidhi
vigezo na kuchaguliwa na MCC kunufaika na msaada wa awamu ya
pili, maandalizi ya mpango huu wa pili (compact II development)
yalianza Aprili 2013 na yatakamilika Septemba 2015. Aidha, mwezi
Novemba 2014, Serikali ya Marekani ilitiliana saini na Serikali ya
Tanzania mkataba wa kutoa Dola za Marekani milioni 9.78 za
kugharamia baadhi ya kazi za maandalizi ya miradi iliyopendekezwa,
hususan upembuzi yakinifu na usadifu katika miradi ya umeme kwa
Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
65. Mheshimiwa Spika, hadi Machi,2015 Dola za Marekani milioni
2.34 zilikuwa zimetolewa na kutumika kwa ajili ya upembuzi yakinifu
na usadifu wa miradi hii ya umeme. Kazi hii inaendelea na inatarajiwa
kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni 2015, ambapo
makadirio ya gharama za mpango huu zitabainishwa kwa maandalizi
ya mkataba wa ufadhili wa miradi hiyo.
Mafao ya Wastaafu na Mirathi
66. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuboresha huduma za
pensheni zinazotolewa moja kwa moja na Wizara yafuatayo
yametekelezwa: kuhakiki idadi halisi ya wastaafu ambapo hadi Aprili,
2015 jumla ya wastaafu 2,273 walihakikiwa na kumbukumbu zao
kuingizwa kwenye daftari. Idadi hii inafanya jumla ya wastaafu
walioingizwa kwenye daftari kufikia 62,126. Aidha, kumbukumbu za
wastaafu zimeendelea kuhifadhiwa kwenye mfumo wa TEHAMA
ambapo kumbukumbu za wastaafu 17,286 ziliwekwa kwenye mfumo
huo.
Mifuko ya Hifadhi za Jamii
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma – PSPF
67. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2015, Mfuko ulikusanya
jumla ya shilingi bilioni 518.13 ambapo kati ya makusanyo hayo,
michango ya wanachama ni shilingi bilioni 334.24 na mapato
yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni 183.89. Aidha, jumla
ya shilingi bilioni 530.38 zilitumika kulipa mafao ikiwa ni pamoja na
mafao ya kiinua mgongo na pensheni za kila mwezi kwa wanachama
6,653. Vile vile, Mfuko ulizindua huduma za Fao la Uzazi, Mkopo wa
Elimu na Mkopo wa Kujipanga Kimaisha ili kuboresha maisha ya
wanachama.
68. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Mfuko unatarajia
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 891.76. Kati ya makusanyo hayo,
michango ya wanachama ni shilingi bilioni 645.81, na mapato
yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni 245.95. Aidha, Mfuko
unatarajia kulipa kiasi cha shilingi bilioni 854.38 kwa ajili ya mafao
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiinua mgongo na pensheni za kila
mwezi, ambapo jumla ya wanachama wapatao 5,445 wanatarajia
kustaafu kwa mujibu wa sheria. Vile vile, Mfuko unatarajia kuwekeza
kiasi cha shilingi bilioni 110.59 kwenye maeneo mbalimbali ya vitega
uchumi.
Mfuko wa Pensheni wa GEPF
69. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 Mfuko umesajili
jumla ya wanachama 13,093 kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi.
Michango ya wanachama ilifikia kiasi cha shilingi bilioni 36.45 sawa
na asilimia 86.56 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 42.11. Mapato
yatokanayo na vitega uchumi yalifikia shilingi bilioni 26.34 ambayo ni
sawa na asilimia 74.91 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 35.10.
Thamani ya Mfuko ilikua na kufikia shilingi bilioni 328.8.
70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Mfuko utaendelea
na jitihada za kuboresha huduma kwa wanachama kwa kutumia
teknolojia ya habari na mawasiliano, kupanua wigo wa wanachama na
kukuza mapato yatokanayo na uwekezaji. Mfuko unatarajia kusajili
jumla ya wanachama 24,020 na kukusanya michango yenye thamani
ya shilingi bilioni 62.21. Aidha, mapato ya vitega uchumi yanatarajiwa
kufikia shilingi bilioni 36 na thamani ya Mfuko inatarajiwa kuwa
shilingi bilioni 537.08.
Mfuko wa Pensheni wa PPF
71. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014, idadi ya wanachama
wapya walioandikishwa ilifikia 67,302 ikilinganishwa na 63,582
mwaka 2013. Michango ya wanachama iliyokusanywa na mfuko ilifikia
shilingi bilioni 335.7 sawa na ongezeko la asilimia 20.5 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 278.5 zilizokusanywa mwaka 2013. Ongezeko hili
limechochewa na kuongezeka kwa mishahara ya wanachama, waajiri
kuzingatia sheria kwa kuleta michango kwa wakati pamoja na
uandikishaji wa wanachama wapya. Aidha, mapato yatokanayo na
uwekezaji yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 318 mwaka 2013 hadi
kufikia shilingi bilioni 361.7 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia
13.7. Thamani ya Mfuko imeongezeka na kufikia shilingi trilioni 1.96
ikiwa ni ongezeko la asilimia 32 ikilinganishwa na thamani ya Mfuko
ya shilingi trilioni 1.49 iliyokuwa mwaka 2013. Vile vile, Mfuko ulilipa
jumla ya shilingi bilioni 156.4 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na
shilingi bilioni 131.9 zilizolipwa mwaka 2013 sawa na ongezeko la
asilimia 18.5.
72. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015, Mfuko unatarajia
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 657.3, kati ya hizo michango ya
wanachama ni shilingi bilioni 400 na mapato yatokanayo na vitega
uchumi ni shilingi bilioni 257.3. Aidha, thamani ya Mfuko inatarajiwa
kufikia shilingi trilioni 2.35. Vile vile, Mfuko unatarajia kuandikisha
wanachama wapya 87,000.
73. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa madeni ya Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ikiwa ni pamoja na yaliyotokana na wastaafu wa
kabla ya mwaka 1999, Serikali iko katika mchakato wa kutoa
hatifungani ya muda mrefu yenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 kwa
mifuko hiyo kwa ajili ya madeni yaliyokwisha iva. Hatifungani hizi
zitatolewa tu baada ya uhakiki kukamilika.
Rufaa za Kodi
74. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2015 Bodi ya Rufaa ya Kodi
imesajili jumla ya rufaa 234 na kutolea maamuzi 65 sawa na asilimia
27.8 ya rufaa zilizosajiliwa. Aidha, Baraza za Rufaa za Kodi limesajili
rufaa 24 na kutolea maamuzi rufaa 26 ikijumuisha rufaa mbili
zilizosajiliwa kabla ya Julai, 2014. Katika mwaka 2015/16 Bodi
itaendelea kusikiliza na kutolea maamuzi rufaa za kodi
zilizowasilishwa na zitakazowasilishwa ili kuhakikisha haki
inapatikana kwa wakati. Bodi pia itaendelea kutoa elimu kwa wadau
ambapo “Tax Law Reports” zitaendelea kutolewa ili ziweze kutumika
kama rejea.
Huduma za Kibenki
Benki Kuu ya Tanzania
75. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2015, sekta ya
benki iliendelea kukua na kuimarika. Idadi ya taasisi za fedha
zinazosimamiwa na Benki Kuu iliongezeka kutoka 57 zilizokuwepo
mwezi Juni, 2014 hadi 59. Aidha, matawi ya benki yaliongezeka
kutoka 634 hadi 698. Katika kipindi hicho, Benki Kuu ilitoa leseni kwa
taasisi nne. Taasisi hizo ni Vision Fund Tanzania Microfinance
Company inayotoa huduma ndogo ndogo za kifedha, Alios Finance
Tanzania Limited ambayo ni Kampuni ya karadha, Salute Finance
Limited, na China Commercial Bank Ltd ambayo ni benki ya biashara.
76. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma za kifedha kwa
wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki umeendelea kuongezeka
kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa huduma za malipo ya
reja reja kupitia simu za mikononi na huduma za uwakala wa mabenki
(agent banking services). Ubunifu huu umechangia kwa kiasi kikubwa
ongezeko la amana za watu binafsi ambazo zimefikia shilingi bilioni
17,904.71 katika kipindi kinachoishia Machi, 2015 kutoka shilingi
bilioni 15,726.5 katika kipindi kama hicho mwaka, 2014. Aidha,
kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea katika utoaji wa
huduma za kibenki, Benki Kuu imefanya marekebisho ya kanuni za
kusimamia mabenki (Prudential Regulations for Banking Institutions)
zilizochapishwa katika gazeti la Serikali la mwezi Agosti, 2014 toleo Na.
290.
77. Mheshimiwa Spika, takwimu za tathmini ya hali ya mabenki
zinaonesha kuwa sekta ya mabenki imeendelea kuwa imara na
salama, ikiwa na mtaji na ukwasi wa kutosha. Katika kipindi
kinachoishia mwezi Machi, 2015, kiwango cha mtaji ikilinganishwa na
mali iliyowekezwa (total capital to total risk weighted assets and
offbalance sheet exposures) kilikuwa cha asilimia 19.09 ikilinganishwa
na kiwango cha chini kinachotakiwa kisheria cha asilimia 12. Vile vile,
ubora wa mikopo uliendelea kuimarika. Uwiano kati ya mikopo
chechefu na jumla ya mikopo yote katika benki za biashara ulipungua
hadi kufikia wastani wa asilimia 6.52 kutoka wastani wa asilimia 8.1
wa mwezi Juni, 2014. Kiwango cha mali inayoweza kubadilishwa kuwa
fedha taslimu ikilinganishwa na kiwango cha amana zinazoweza
kuhitajika katika muda mfupi (Liquid assets to demand liabilities)
kilifikia asilimia 37.52 ikilinganishwa na asilimia 35.61 mwezi Juni,
2014 na kiwango kinachohitajika kisheria cha asilimia 20 au zaidi.
78. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Tanzania imejiunga
na mfumo wa malipo wa Jumuiya ya nchi za SADC ujulikanao kama
SADC Intergrated Regional Electronic Settlement System (SIRESS) ili
kurahisisha biashara na uwekezaji katika Jumuiya hiyo na hivyo
kupanua wigo wa watanzania kufanya biashara kimataifa. Aidha,
maboresho katika mfumo wa malipo kwa hundi unaendelea ambapo
hadi kufikia Aprili,2015 mfumo mpya wa Tanzania Automated Clearing
System umeanza kutumika badala ya mfumo uliokuwepo awali.
Maboresho haya yameongeza ufanisi mkubwa na kupunguza muda wa
kusubiri malipo ya hundi kutoka siku tatu mpaka saba hadi siku
moja.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo
79. Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha taratibu za kuanzisha
Benki hii na hatua zifuatazo zimeshakamilika: ofisi kwa ajili ya kuanza
shughuli za Benki hiyo imeshapatikana; Bodi ya Wakurugenzi
imeshaundwa na kuanza kazi rasmi tangu Februari 2014; Mkurugenzi
Mkuu na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa Benki hiyo
wameshateuliwa na kuajiriwa na tayari wameshaanza kazi tangu
Septemba 2014; baadhi ya Mameneja wameshaajiriwa na taratibu za
kuwaajiri maafisa wengine wa ngazi mbalimbali za chini zinaendelea
vizuri; leseni ya muda ya kuanzisha Benki hiyo ya maendeleo ya kilimo
imeshatolewa na Benki Kuu ya Tanzania na taratibu za kukamilisha
masharti ya upatikanaji wa leseni ya kudumu ya shughuli za kibenki
zinaendelea na uzinduzi rasmi unatarajiwa kufanyika mwezi Julai,
2015.
80. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2015/16, benki imepanga
kufanya yafuatayo: kupata leseni ya kudumu ya huduma za kibenki
toka Benki Kuu ya Tanzania; kuzindua rasmi benki na kuanza kutoa
mikopo ya maendeleo ya kilimo; kukamilisha ajira za wafanyakazi 45
waliokusudiwa kuanzisha benki; na kukamilisha Mpango Kazi,
miundo ya uendeshaji na mipango ya utekelezaji ya mwaka.
Benki ya Posta Tanzania
81. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014 Benki ya Posta
iliendelea kusambaza huduma zake za kibenki kwa wananchi wengi
zaidi ambapo hadi Disemba 2014 jumla ya matawi 28 na matawi
madogo 22 yalikuwa yanatoa huduma kwa wananchi. Aidha, amana za
wateja ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 169.29 mwaka 2013 hadi
kufikia shilingi bilioni 237.53 mwaka 2014 sawa na ongezeko la
asilimia 40. Thamani ya mikopo inayotolewa kwa wateja iliongezeka
kutoka shilingi bilioni 120.42 mwaka 2013 hadi kufikia shilingi bilioni
215.41 mwaka 2014 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 79. Pato
ghafi lililozalishwa na benki liliongezeka toka shilingi bilioni 38.36
mwaka 2013 na kufikia shilingi bilioni 52.77 mwaka 2014.
82. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015, Benki ya Posta
imejipanga kimkakati ili kuukabili ushindaji wa kibiashara katika soko
la fedha na kuongeza uwezo wake wa uzalishaji na utoaji huduma kwa
kufanya yafuatayo: kuongeza mtaji kwa kubadili sheria iliyoianzisha ili
kufungua milango kwa kuongeza wanahisa wengine kupitia soko la
mitaji; kupanua huduma kwa wateja wengi zaidi kwa kutumia
teknolojia ya TPB POPOTE; kufungua akaunti za wateja wapya
200,000; kufungua matawi madogo madogo manane wilayani ili
kuwafikia wateja wengi zaidi; na kuongeza bidhaa za kibenki.
Benki ya Maendeleo TIB
83. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014 Benki ya Maendeleo
TIB ilikamilisha mpango wake wa marekebisho na kupata leseni kwa
makampuni mawili ya TIB. Katika kipindi kilichoishia Disemba, 2014
Benki ilipata faida kabla ya kodi ya shilingi bilioni 10.4 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 11.6 zilizopatikana mwaka 2013. Kupungua kwa
faida kumetokana na tengo la mikopo chechefu kulingana na kanuni
za kibiashara. Aidha, waraka mizania wa benki ulikua na kufikia
shilingi bilioni 520.1 sawa na ongezeko la asilimia 24.5 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 417.9 mwaka 2013. Vile vile, mikopo iliyotolewa
katika sekta za ujenzi, biashara, utalii, afya, elimu na SMEs ilifikia
shilingi bilioni 413.0 sawa na ongezeko la asilimia 35 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 305.8 mwaka 2013.
84. Mheshimiwa Spika, dirisha la kilimo liliendelea kutoa mikopo
kwa wakopaji mbalimbali kwa riba nafuu. Tangu kuanza kwa dirisha
mwaka 2010 hadi kufikia Disemba, 2014 maombi yenye thamani ya
shilingi bilioni 299.1 yalipokelewa. Kati ya hayo, maombi ya shilingi
bilioni 67.5 yaliidhinishwa. Waombaji waliopata mikopo wanatoka
kwenye mikoa 22 ambayo ni Arusha, Pwani, Simiyu, Kagera, Mara,
Dodoma, Mwanza, Geita, Kilimanjaro, Manyara, Dar Es Salaam,
Singida, Iringa, Morogoro, Tanga, Mbeya, Unguja, Mtwara, Ruvuma,
Njombe, Rukwa na Kigoma. Kati ya mikopo hiyo, shilingi bilioni 28.1
(asilimia 54) zilitolewa kwa wakulima wadogo na wa kati wenye
kampuni, shilingi bilioni 7.6 (asilimia 14.6) zilitolewa kwa taasisi ndogo
za fedha zinazokopesha wakulima wadogo na wa kati na shilingi bilioni
16.4 (asilimia 28.3) zilitolewa kwa vikundi vya kuweka na kukopa.
Twiga Bancorp
85. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014 Twiga Bancorp
imeendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki ambapo hadi
Disemba, 2014 amana za wateja zilifikia shilingi bilioni 57
ikilinganishwa na shilingi bilioni 53 mwaka 2013. Aidha, mikopo
iliyotolewa kwa wateja mbalimbali ilifikia shilingi bilioni 42 ikiwa ni
pungufu kwa asilimia 5 ikilinganishwa na mikopo iliyotolewa mwaka
2013. Kushuka kwa mikopo kunatokana na nguvu nyingi kuelekezwa
kwenye ukusanyaji wa mikopo chechefu.
86. Mheshimiwa Spika, benki kwa mwaka 2015 imepanga kufanya
yafuatayo: kuongeza amana za wateja kutoka shilingi bilioni 57 hadi
shilingi bilioni 77; kukuza mikopo ya taasisi kutoka shilingi bilioni 42
mwaka 2014 hadi shilingi bilioni 55; na kuongeza mapato ya taasisi
kwa asilimia 40 kutokana na riba na mapato mengine yasiyo ya riba.
Huduma za Bima
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima
87. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Bima imeanzisha Baraza la
usuluhishi la Bima na linaendelea kupokea malalamiko ya wateja wa
bima na kuyatolea ufumbuzi ili kukuza imani kwa Wananchi kuhusu
huduma za bima. Aidha, Mamlaka kwa kushirikiana na wadau
wengine, imeendelea kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa
na bima hususan Bima ya moto na majanga mengine. Lengo ikiwa
ifikapo mwaka 2017 asilimia 25 ya Watanzania wote wawe wamefikiwa
na huduma za bima.
88. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Mamlaka itafungua
Ofisi ya Kanda ya Kati itakayohudumia mikoa ya Singida, Tabora na
Dodoma. Lengo ni kupeleka huduma za Mamlaka karibu zaidi na
Wananchi. Aidha, Mamlaka itaendelea kutoa elimu ya bima kwa umma
kwa njia ya redio. Vile vile, Mamlaka itashirikiana na vyuo vikuu vya
ndani na nje ya nchi kutoa elimu ya juu kwa lengo la kupata wataalam
wengi wa fani ya bima.
Shirika la Bima la Taifa
89. Mheshimiwa Spika, mapato ya shirika kutokana na ada za bima
yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 31.5 mwaka 2013 hadi shilingi
bilioni 31.7 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.6. Aidha,
mapato ya shirika kutokana na bima mtawanyiko yaliongezeka kutoka
shilingi bilioni 1.7 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 1.77 mwaka 2014
sawa na ongezeko la asilimia 4.1. mapato yatokanayo na vitega
uchumi yalipungua kutoka shilingi bilioni 7.3 mwaka 2013 hadi
shilingi bilioni 6.3 mwaka 2014 ikiwa ni sawa na upungufu wa asilimia
14.7.
90. Mheshimiwa Spika, katika kipindi kilichoishia 31 Desemba
2014, Shirika liliweza kulipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 9.8
ikiwa ni asilimia 75 ya lengo la mwaka 2014. Kati ya kiasi hicho
shilingi bilioni 6.4 zililipwa kwa wateja wa bima za maisha na shilingi
bilioni 3.4 zililipwa kwa wateja wa bima zisizo za maisha.
91. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015, shirika limejiwekea
lengo la kukusanya mapato ya shilingi bilioni 68.9. Kati ya hayo,
shilingi bilioni 49.3 zitatokana na ada ya bima na shilingi bilioni 19.5
zitatokana na vitega uchumi vya shirika, ada za bima mtawanyo na
uuzaji wa nyumba na viwanja. Aidha, shirika litaendelea na mkakati
wa kuzishawishi Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma kununua
bima mbalimbali kutoka shirika la Bima la Taifa ili kuliwezesha
kuongeza mapato.
Mitaji na Dhamana
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana
92. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana
imetekeleza yafuatayo: kusimamia Soko la Hisa la Dar es Salaam,
kampuni za udalali wa uwekezaji, Mipango ya uwekezaji wa pamoja na
kampuni zinazomilikiwa na wanahisa wengi; kukagua madalali na
washauri wa uwekezaji ili kuona kama wanafuata sheria na taratibu
zilizowekwa; na kuchambua taarifa mbalimbali kuhusu Mipango ya
uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS ili kuona kama
wanafuata taratibu na sheria. Aidha, Mamlaka iliendelea kutoa elimu
kwa umma kuhusu fursa za uwekezaji na faida za kuwekeza katika
Masoko ya Mitaji nchini Tanzania.
93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Mamlaka itaandaa
taratibu za kisheria na usimamizi wa bidhaa na Huduma mpya
zinazotarajiwa kuingizwa sokoni. Bidhaa hizo ni Hatifungani za
Manispaa, mifuko ya uwekezaji iliyoorodheshwa sokoni (Exchange
Traded Funds), na hatifungani za akiba kwa ajili wawekezaji wadogo
kwa kutumia mitandao ya simu za mikononi (Makiba Bonds).
Soko la Hisa la Dar es Salaam
94. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2015 Soko la Hisa la Dar es
Salaam limeorodhesha hatifungani za Serikali zenye thamani ya
shilingi bilioni 862.53. Kwa upande wa hisa za kampuni, Soko
liliorodhesha hisa za kampuni za Swala Oil and Gas ltd, Uchumi Super
Market na Mkombozi Commercial Bank. Aidha, hisa za benki ya
walimu-Mwalimu Commencial Bank zilianza kuuzwa katika soko la
awali.
95. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2015 hisa zenye thamani ya
shilingi bilioni 651.9 ziliuzwa na kununuliwa. Kwa upande wa
hatifungani za Serikali, hatifungani zenye thamani ya shilingi bilioni
401.78 ziliuzwa. Aidha, mauzo ya hisa yameongezeka kutoka shilingi
bilioni 251.20 mwaka 2013/14 hadi shilingi bilioni 651.9 mwaka
2014/15, sawa na ongezeko la asilimia 160. Thamani ya Soko imekua
kutoka shilingi trilioni 17.3 hadi shilingi trilioni 22.7. sawa na
ongezeko la asilimia 31. Mafanikio haya yametokana na kuongeza
ufanisi katika uendeshaji wa soko, elimu kwa umma, na utendaji
mzuri wa kampuni zilizoorodheshwa.
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania
96. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka miwili tangu
kuanzishwa kwake, Kampuni ya UTT AMIS, ikiwa kama meneja wa
mifuko ya uwekezaji wa pamoja ilijikita zaidi katika kuimarisha,
kuboresha na kukuza mifuko mitano iliyorithi toka UTT ili iweze
kutimiza malengo yake. Mifuko hiyo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa
Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Jikimu na Mfuko wa
Ukwasi. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, 2015 mifuko hii
ilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi bilioni 237 ikilinganishwa na
kiasi cha shilingi bilioni 166.1 mwezi Machi 2014 na wawekezaji zaidi
ya 120,000.
97. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo
Tanzania (UTT MFI) yenye makao makuu Dar es Salaam na ofisi za
kanda zilizopo Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza, na Zanzibar. Taasisi
imejikita katika kutoa huduma za kifedha na mikopo kwa watanzania
wenye kipato cha chini na cha kati. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2015
jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 6.09 ilitolewa kwa wananchi 11,591
kati ya hao wanawake ni 9,263 na wanaume ni 2,328. Aidha, pamoja
na mikopo inayotolewa na UTT MFI, taasisi hii pia inatoa huduma za
uuzaji wa vipande vya UTT AMIS.
98. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundombinu (UTT-Projects and Infrastructure Development) imejikita
katika upimaji wa ardhi na kuhakikisha kuwa wananchi wote
wanapata ardhi iliyopimwa. Hadi mwezi Aprili 2015, taasisi imepima
viwanja katika maeneo ya Sengerema, Mapinga, Lindi, Morogoro, na
Bukoba na kutoa ushauri wa namna bora ya kuendesha na
kusimamia soko la Mwanjelwa mkoani Mbeya. Katika mwaka
2015/16, taasisi imepanga kukuza mtaji, kutoa elimu kwa umma
kuhusu umuhimu wa makazi yaliyopangwa, na kuboresha
miundombinu ya taasisi.
Taasisi za Mafunzo
99. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na taasisi za
mafunzo zilizo chini yake, imeendelea kutoa taaluma mbalimbali
nchini. Taasisi hizo ni Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA); Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA); Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo
cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP); na Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC). Katika kutekeleza jukumu hili taasisi
za mafunzo zimeendelea kudahili wanafunzi na kutoa mafunzo katika
taaluma mbalimbali nchini, kuanzisha kozi mpya ili kukidhi mahitaji
ya soko la ajira la ndani na nje ya nchi, kupanua huduma za mafunzo
ili kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya elimu
pamoja na kuendelea kuwekeza katika miundo mbinu mbalimbali ya
taasisi hizi ili kuendana na ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kila
mwaka.
100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, udahili wa
wanafunzi ulikuwa kama ifuatavyo: Taasisi ya Uhasibu Arusha
wanafunzi 3,675; Taasisi ya Uhasibu Tanzania wanafunzi 8,644; Chuo
cha Usimamizi wa Fedha wanafunzi 9,779; Chuo cha Mipango na
Maendeleo Vijijini wanafunzi 5,030; na Chuo cha Takwimu Mashariki
mwa Afrika wanafunzi 400.
101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 kozi mpya mbili
zimeanza kufundishwa katika Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini
ambazo ni: Certificate in Development Administration and Management
na Diploma in Development Administration and Management. Vile vile,
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, kimeendesha mafunzo ya
awali kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa takwimu wanafunzi
waliomaliza elimu ya Sekondari na hawakufanikiwa kuingia Kidato cha
Tano. Aidha, Taasisi ya Uhasibu Arusha imeanzisha kozi mpya za
shahada ya Uzamili katika Ugavi na shahada ya Mafunzo Mkakati na
kufungua kampasi katika mji wa Babati mkoani Manyara na jijini
Mwanza.
102. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa 2015/16, Wizara itaendelea
kushirikiana na taasisi zake katika kudahili wanafunzi, kuboresha
miundombinu pamoja na kuanzisha kozi zenye kukidhi mahitaji ya
soko la ajira.
Taasisi za Kitaalam na Huduma Nyinginezo
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi
103. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutimiza majukumu
yake kupitia Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi – NBAA kama
ifuatavyo: kusimamia utumiaji wa viwango vya kimataifa vya
utayarishaji na ukaguzi wa taarifa za hesabu nchini; kuhariri mitaala
pamoja na silabi ya taaluma ya uhasibu; kuendeleza taaluma ya
uhasibu; kufanya usajili wa wahasibu na kutunza takwimu; kuweka
na kusimamia viwango vya uhasibu na ukaguzi; kusimamia ubora wa
ukaguzi wa hesabu (audit quality review) ambapo hadi Aprili, 2015
NBAA imefanya ukaguzi katika kampuni 34 kati ya kampuni 39
uliopangwa kufanyika kwa kipindi hicho.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
104. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutimiza majukumu
yake kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu – NBS ya kukusanya,
kuchambua, kutunza na kuwasilisha takwimu zilizohitajika katika
sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama ifuatavyo: kuhakiki
Mipaka ya Kiutawala kwa wilaya za Gairo, Chemba, Wete na Kiteto
kwa lengo la kuboresha kanza ya kijiografia inayotokana na Sensa ya
Watu na Makazi ya mwaka 2012 kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya
Mwaka 2022; kuhakiki mipaka ya utawala katika ngazi ya vijiji/mitaa
katika wilaya za Bagamoyo na Kiteto; na kutoa Takwimu za Pato la
Taifa kwa kila robo mwaka na nusu mwaka, takwimu hizo zimetolewa
hadi kufikia Desemba, 2014.
105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Serikali kupitia
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilifanya marekebisho ya takwimu za Pato la
Taifa kwa kutumia mwaka 2007 kama mwaka wa kizio kutoka mwaka
wa kizio wa 2001. Mwaka 2007 umetumika kwa vile ulikuwa na taarifa
nyingi kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tafiti za
kiuchumi, kijamii na taarifa za kiutawala. Umuhimu wa marekebisho
hayo unatokana na maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko ya sayansi
na teknolojia. Mabadiliko hayo yamesababisha kuwepo kwa haja ya
kufanya marekebisho na kujumuisha thamani ya bidhaa na huduma
mpya katika Pato la Taifa ambazo hapo awali hazikuwepo – mfano gesi
asilia, sanaa na burudani na kuongezeka kwa matumizi ya vifaa vya
elekroniki zikiwemo simu za kiganjani.
106. Mheshimiwa Spika, kutokana na marekebisho hayo, ukuaji
halisi wa Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007 ulikuwa asilimia 7.3
mwaka 2013 ikilinganishwa na asilimia 5.3 mwaka 2012. Aidha, Pato
la Taifa kwa mwaka 2013 kabla ya marekebisho hayo lilikuwa shilingi
trilioni 53.2. Baada ya marekebisho hayo, ilionekana kuwa Pato la
Taifa lilikuwa shilingi trilioni 70 mwaka 2013 sawa na ongezeko la
asilimia 31.6. Vivyo hivyo, wastani wa Pato la kila Mtanzania kwa
mwaka 2013 lilikuwa shilingi 1,582,797 badala ya shilingi 1,186,200
kama ilivyokisiwa awali. Kufikia mwaka 2014, Pato la Taifa lilikua na
kufikia shilingi trilioni 79.4 na wastani wa pato la kila mtu lilikuwa
shilingi 1,724,416 (wastani wa Dola za Marekani 1,066).
107. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa takwimu hizo mpya,
kiwango halisi cha ukuaji wa uchumi kilikuwa asilimia 7.0 mwaka
2014 ikilinganishwa na asilimia 7.3 mwaka 2013. Katika kipindi hicho,
shughuli za uchumi zilizokua kwa viwango vikubwa zilikuwa ni pamoja
na: ujenzi (asilimia 14.1); usafirishaji na uhifadhi (asilimia 12.5); fedha
na bima (asilimia 10.8); biashara (asilimia 10.0); na viwanda (asilimia
9.4). Aidha, kiwango cha ukuaji wa sekta ya kilimo mwaka 2014
kilikuwa kidogo (asilimia 3.4) pamoja na kwamba sekta hii inaongoza
kwa kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa kwa asilimia 28.9.
Sekta zinazofuata kwa mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa ni
ujenzi (asilimia 12.5); biashara (10.5); na viwanda (asilimia 5.6).
108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha iliendelea kusimamia michezo ya kubahatisha nchini
ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi (gaming tax) itokanayo na michezo
ya kubahatisha. Hadi Aprili, 2015 jumla ya shilingi bilioni 12.63
zilikusanywa sawa na asilimia 99.63 ya lengo. Kiasi hiki ni sawa na
ongezeko la asilimia 14.62 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi
bilioni 10.78 katika kipindi cha mwaka 2013/14. Aidha, Bodi
ilichangia shilingi milioni 623.67 katika Mfuko Mkuu wa Serikali; sawa
na ongezeko la asilimia 17.13 ikilinganishwa na shilingi milioni 532.48
ya mwaka 2013/14.
109. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Bodi imefanya
utafiti kubaini athari ya kiuchumi na kijamii kutokana na uwepo wa
michezo ya kubahatisha na hasa katika jiji la Dar es Salaam.
Mapendekezo yaliyotokana na utafiti huo yamesaidia Bodi katika
kuboresha utaratibu wa utoaji wa leseni mbalimbali ili kuhakikisha
kwamba sekta inachangia zaidi katika maendeleo ya kiuchumi na
kijamii. Aidha, katika mwaka 2015/16 Bodi inatarajia kukusanya
mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 13.50 na hivyo kuchangia kiasi cha
Shilingi bilioni 1.35 kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Mapitio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara kwa Mwaka
2014/15
FUNGU 50 – Wizara ya Fedha
110. Mheshimiwa Spika, Wizara ilikadiria kukusanya shilingi bilioni
2.53 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato yasiyo ya kodi. Vyanzo
hivyo ni pamoja na mauzo ya nyaraka za zabuni, leseni za minada na
pango kutoka kwenye mashirika ya umma na taasisi za Serikali. Hadi
kufikia tarehe 30 Aprili, 2015 mapato yasiyo ya kodi yalifikia shilingi
milioni 680.36 sawa na asilimia 27 ya makadirio.
111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Fungu 50
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 66.67 kwa ajili ya
Matumizi ya Kawaida. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 5.62 ni kwa
ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 61.05 ni kwa ajili ya
Matumizi Mengineyo. Hadi kufikia Aprili, 2015, Matumizi ya Kawaida
yalifikia shilingi bilioni 39.43. sawa na asilimia 59 ya makadirio. Kati
ya hizo shilingi bilioni 3.52 ni malipo ya mishahara kwa watumishi wa
fungu hili na shilingi bilioni 35.90 ni matumizi mengineyo.
112. Mheshimiwa Spika, bajeti ya matumizi ya maendeleo ilikuwa
shilingi bilioni 29.80. Hadi kufikia Aprili, 2015 matumizi ya
maendeleo yalikuwa shilingi bilioni 9.26 ikiwa ni sawa na asilimia 31
ya makadirio ya matumizi ya maendeleo.
Fungu 21- HAZINA
113. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Fungu 21
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 897.05. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 4.04 ni kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni
662.43 ni matumizi maalum, shilingi bilioni 201.64 ni kwa ajili ya
ruzuku ya vyuo na taasisi zilizo chini ya Hazina na shilingi bilioni
28.94 ni matumizi mengineyo ya idara zilizo chini ya Fungu hili.
114. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 matumizi ya
kawaida yalikuwa ni shilingi bilioni 588.42. Kati ya fedha hizo, shilingi
bilioni 2.63 zilitumika kulipia mishahara ya watumishi waliopo chini
ya Fungu 21, shilingi bilioni 13.44 zimetumika katika matumizi
mengineyo ya idara, shilingi bilioni 150.49 zilitumika kulipia ruzuku
ya vyuo na taasisi na shilingi bilioni 421.86 ni matumizi maalum.
115. Mheshimiwa Spika, bajeti ya fungu 21 kwa ajili ya matumizi ya
maendeleo ilikuwa ni shilingi bilioni 57.37. Kati ya kiasi hicho, shilingi
bilioni 40.37 ni fedha za nje, na shilingi bilioni 17.00 ni fedha za
ndani. Hadi Aprili, 2015 matumizi ya fedha za maendeleo yalifikia
shilingi bilioni 28.29 sawa na asilimia 49 ya makadirio.
Fungu 22 – Deni la Taifa
116. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Fungu 22
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 4,354.86. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 6.58 ni kwa ajili ya mishahara na stahili za
maafisa wa Serikali wa kada maalum, shilingi bilioni 4,348.28 ni kwa
ajili ya kulipia Deni la Taifa, pensheni, michango ya mwajiri kwenye
mifuko ya hifadhi ya jamii na matumizi mengineyo. Hadi Aprili, 2015
matumizi ya fungu hili yalifikia shilingi bilioni 3,595.75. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 3.85 ni mishahara na shilingi bilioni 3,591 nie
kwa ajili ya malipo ya Deni la Taifa, pensheni na michango ya mwajiri
katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali
117. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Fungu 23
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 80.11. Kati ya kiasi
hicho, mishahara ni shilingi bilioni 5.01 na shilingi bilioni 75.1 ni kwa
ajili ya matumizi mengineyo. Hadi Aprili, 2015 matumizi ya kawaida
yalikuwa shilingi bilioni 47.93 sawa na asilimia 59 ya bajeti ya
matumizi ya kawaida.
118. Mheshimiwa Spika, bajeti ya fungu 23 kwa ajili ya matumizi ya
maendeleo ilikuwa shilingi bilioni 7.95. Hadi Aprili, 2015 matumizi
yalifikia shilingi bilioni 1.98 sawa na asilimia 24 ya bajeti.
Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha:
119. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Fungu 10
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 2.32. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 0.42 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na
shilingi bilioni 1.9 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo. Hadi Aprili,
2015, matumizi yalifikia shilingi bilioni 1.14.
Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu
120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Fungu 13
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 0.19 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo. Hadi Aprili, 2015, matumizi ya kawaida yalikuwa shilingi
bilioni 1.1 sawa na asilimia 69 ya fedha zilizoidhinishwa.
Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina
121. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizara kupitia
Ofisi ya Msajili wa Hazina ilikadiria kukusanya jumla ya Shilingi
bilioni 144.22 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato yasiyo ya kodi
ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 10 na marejesho
ya mikopo na riba kutoka kwenye taasisi na mashirika ya umma. Hadi
kufikia Aprili, 2015, makusanyo yalifikia shilingi bilioni 128.6, sawa na
asilimia 89.2 ya lengo la mwaka. Kati ya fedha hizo makusanyo
yatokanayo na gawio yalikuwa shilingi bilioni 24.5 na michango ya
taasisi kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali ilifikia shilingi bilioni 41.7.
Aidha, mapato yatokanayo na marejesho ya mikopo yalikuwa shilingi
milioni 805.3.
122. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Fungu 7
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 142.43. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 0.67 ni kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni
3.76 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi bilioni 137.99 ni
kwa ajili ya matumizi maalum. Hadi Aprili, 2015 matumizi ya kawaida
yalifikia shilingi bilioni 139.12 sawa na asilimia 97 ya bajeti ya
matumizi ya kawaida. Kati ya matumizi hayo mishahara ni shilingi
bilioni 0.65 na matumizi mengineyo ni shilingi bilioni 2.12 na shilingi
bilioni 136.36 ni kwa ajili ya ulipaji madeni ya kimkataba na
urekebishaji wa mashirika na taasisi.
49 | P a g e
123. Mheshimiwa Spika, bajeti ya Fungu 7 kwa ajili ya matumizi ya
maendeleo ilikuwa shilingi bilioni 1.94. Hadi Machi, 2015 matumizi ya
maendeleo yalifikia shilingi bilioni 0.68 sawa na asilimia 34 ya
makadirio.
Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
124. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Fungu 45
liliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 65.97 kwa ajili ya
Matumizi ya Kawaida. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 10.41 ni kwa
ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 55.56 ni kwa ajili ya
Matumizi Mengineyo. Hadi kufikia Aprili, 2015, Matumizi ya Kawaida
yalifikia shilingi bilioni 31.86 sawa na asilimia 48 ya makadirio.
125. Mheshimiwa Spika, bajeti ya matumizi ya maendeleo ilikuwa
shilingi bilioni 7.08. Hadi kufikia Aprili, 2015 matumizi ya maendeleo
yalikuwa shilingi bilioni 7.08 ikiwa ni sawa na asilimia 100 ya
makadirio ya matumizi ya maendeleo.
CHANGAMOTO
126. Mheshimiwa Spika, Wizara katika kutekeleza majukumu yake
ilikabiliwa na changamoto zifuatazo:-
i. Kutofikiwa kwa lengo la ukusanyaji wa mapato;
ii. Kuchelewa kupatikana kwa fedha zilizoahidiwa na wafadhili;
iii. Wafanyabiashara kugomea matumizi ya mashine za kielekroniki
za kutolea risiti (EFDs);
iv. Mchakato mrefu wa kupata mikopo ya kibiashara; na
v. Uelewa wa jamii, sekta binafsi na sekta ya umma kuhusu
uendelezaji wa miradi iliyo katika Ubia wa Sekta ya Umma na
Sekta binafsi.
127. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo,
Wizara imechukua hatua zifuatazo:
i. Kuendelea kusimamia mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili
kupunguza utegemezi;
ii. Kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi
na faida za mashine za kielekroniki za kutolea risiti (EFDs); na
iii. Kutoa elimu kwa umma na wawekezaji kuhusu dhana ya Ubia wa
Sekta ya Umma na Sekta binafsi.
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/16
MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
Mapato
Fungu 50: Wizara ya Fedha
128. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizara ya Fedha
Fungu 50 inakadiria kukusanya mapato yasiyo ya kodi yapatayo
shilingi 2,528,002,000 (bilioni 2.53)
Maombi ya Fedha
Fungu 50 – Wizara ya Fedha.
129. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 71,036,206,000 (bilioni 71.03).
Kati ya hizo:
(i) Mishahara – Shilingi 7,624,532,000 (bilioni 7.6)
(ii) Matumizi mengineyo – Shilingi 63,411,674,000
(bilioni 63.41)
(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 370,544,428,000
(bilioni 370.54). Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani – Shilingi 12,000,000,000 (bilioni 12).
(ii) Fedha za Nje – Shilingi 358,544,428,000 (bilioni 358.54).
Fungu 21 – HAZINA:
130. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 551,448,351,000 (bilioni
551.45). Kati ya hizo:
(i) Mishahara – Shilingi 62,404,177,000 (bilioni 62.4) kwa
ajili ya kulipa Mishahara ya watumishi wa Idara/ Vitengo
vilivyo chini ya Fungu hili pamoja na nyongeza ya
mishahara ya Watumishi wa Serikali.
(ii) Matumizi Mengineyo – Shilingi 489,044,174,000
(bilioni 489.04) kwa ajili ya matumizi ya idara, taasisi zilizo
chini ya Fungu hili, na matumizi maalum.
(b) Miradi ya maendeleo – Shilingi 680,960,366,000
(bilioni 680.96). Kati ya hizo:
52 | P a g e
(i) Fedha za Ndani – Shilingi 671,926,000,000 (bilioni 671.93)
(ii)Fedha za Nje – Shilingi 9,034,366,000 (bilioni 9.03)
Fungu 22- Deni la Taifa
131. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 6,254,871,977,000
(bilioni 6,254.87). Kati ya hizo:
(i) Mishahara – Shilingi 9,031,287,000 (bilioni 9.03)
(ii) Matumizi mengineyo – Shilingi 6,245,840,690,000
(bilioni 6,245.84)
Fungu 23 – Mhasibu Mkuu wa Serikali:
132. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 85,438,477,000 (bilioni
85.44). Kati ya hizo
(i) Mishahara – Shilingi 7,932,329,000 (bilioni 7.93)
(ii) Matumizi mengineyo – Shilingi 77,506,148,000
(bilioni 77.51).
(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 4,673,845,000 (bilioni 4.67)
Kati ya hizo:
(i) Fedha za ndani – Shilingi 3,000,000,000 (bilioni 3).
(ii) Fedha za Nje – Shilingi 1,673,845,000 (bilioni 1.67).
Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina:
133. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 27,257,676,000 (bilioni
27.26). Kati ya hizo:-
(i) Mishahara – Shilingi 2,649,137,000 (bilioni 2.65)
(ii) Matumizi mengineyo- Shilingi 24,608,539,000 (bilioni 24.61).
(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 999,885,000 (bilioni 0.99) Kati
ya hizo:
(i) Fedha za ndani -Shilingi 650,000,000 (bilioni 0.65).
(ii) Fedha za Nje -Shilingi 349,885,000 (bilioni 0.34).
Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha:
134. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
(a) Matumizi ya Kawaida – Shilingi 2,439,537,000 (bilioni 2.43)
Kati ya hizo:-
(i) Mishahara – Shilingi 904,792,000 (bilioni 0.90)
(ii) Matumizi mengineyo – Shilingi 1,534,745,000 (bilioni 1.53).
Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu:
135. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 1,534,745,000 (bilioni 1.53).
(b) Miradi ya Maendeleo, fedha za nje – shilingi 35,768,000
(milioni 35.77).
Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
136. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka 2015/16,
Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)Matumizi ya kawaida shilingi 72,152,770,000 (bilioni 72.15).
Kati ya hizo mishahara ni shilingi 14,209,821,000
(bilioni 14.21) na matumizi mengineyo ni shilingi
57,942,949,000 (bilioni 57.94)
(b)Miradi ya Maendeleo shilingi 10,667,116,000. Kati ya hizo:
(i) Fedha za Ndani shilingi 8,000,000,000 (bilioni 8)
(ii) Fedha za Nje shilingi 2,667,116,000 (bilioni 2.66)
HITIMISHO
137. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru
Naibu Mawaziri, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mhe. Adam
Kighoma Ali Malima (Mb). Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati
kwa Katibu Mkuu Dkt. Servacius B. Likwelile na Manaibu wake
Profesa Adolf F. Mkenda, Bibi Dorothy S. Mwanyika na Dkt. Hamisi H.
Mwinyimvua kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia utekelezaji
wa majukumu ya Wizara. Vile vile, napenda kuwashukuru Bw.
Richard L. Mkumbo, Mkurugenzi wa Mipango kwa kuratibu vema
maandalizi ya bajeti ya wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo,
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha pamoja na Wakuu wa Taasisi na
Wakala wa Serikali zilizo chini ya Wizara ya Fedha kwa michango yao
mikubwa katika kuandaa hotuba hii.
138. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Waheshimiwa
Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika
tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz)