Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa kwa ajiri kuwafundisha vijana ambao ni maalumu kwa ajili ya kuwa waalimu watakao wafundisha wanafunzi katika kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo, Mgunga Mwamnyenyelwa ameeleza jinsi kituo hicho kilivyo weza kuanzishwa katika maeneo ya Mburahati na wakazi wa maeneo hayo kuweza kufaidika na kituo hicho, vilevile ameeleza changamoto wanazo kumbana nazo katika kituo hicho.
Mradi huo wa FFL unao fadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) unaendeshwa kwa hisani ya Goethe-Institute kama Msimamizi Mkuu ambapo Meneja wa mradi, Habiba Issa ameeleza jinsi mradi huo unavyo endeshwa ikiwa lengo la mradi huu ni kuendeleza kukuza kwa vipaji kwa vijana na kuweza kujipatia fura mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa mwalimu katika sehemu tofauttofauti za mradi huo
Aidha Meneja huyo Habiba Issa alisema kuwa wameamua kuanzisha mrahi huu wa ili kuweza kuwasaidia vijana hususani walio maliza katika viwango mbalimbali vya elimu kwani wameweza kuwaandalia mazingira mazuri ya kujifunza uselemala, utengenezaji wa maleba (costomes) kwaajili ya sanaa,uandaaji wa jukwaa (stage desgn) na matumizi ya mfumo wa sauti na mwanga katika maonyesho ya sanaa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Baba watoto, Bw. Mgunga na Meneja Mradi wa FIT For the Fit, Habiba Issa wametoa rai kwa wazazi na vijana mbalimbali kutumia fursa zinazo onekana ili kufikia malengo yao. Aidha waliweza kutoa mifano mbalimbali ambapo waliwataja wahitimu walio kuwa waalimu na wengine kutoka nje ya nchi ikiwa ni idadi zaidi ya wanafunzi watano ambao waliweza kwenda nchini India na nchi nyingine za jirani.
Viongozi wa mradi pia waliwataka wazazi kuwa na moyo wa kuwaleta watoto katika kituo hicho ili waweze kupata elimu ya sanaa mbalimbali waache dhana potofu ya kufikiri kwamba sanaa ni uhuni usio kuwa na faida.