Baba Mzazi wa Wema Sepetu Afariki Dunia Dar

Wema Sepetu

Wema Sepetu

BABA mzazi wa aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Balozi Issac Sepetu amefariki dunia leo asubuhi jijini Dar es Salaam. Mzee Issac Sepetu amefariki dunia katika hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa zaidi zinasema Mzee Sepetu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari pamoja na kiharusi. Taarifa zaidi juu ya msiba huu ni hapo baadaye. Hili ni pigo kubwa kwa Wema Sepetu mwanadada mrembo, muigizaji wa filamu nchini ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi ya wazazi wake.

Mtandao wa dev.kisakuzi.com inatoa pole kwa wafiwa wote, wanafamilia, ndugu na marafiki walioguswa na msiba huu.