Baadhi ya Wajumbe Bunge la Katiba Wataka Serikali Mbili

Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalum la Katiba Ummy Ally Mwalimu (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu maendeleo waliyofikia katika kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.  Kulia ni Makamu wake Profesa Makame Mbarawa.

Na Magreth Kinabo – Maelezo Dodoma

BAADHI ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamependekeza kuwepo kwa Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye mfumo wa Serikali mbili, wakati wa kuchambua sura ya kwanza na ya sita zilizoko katika Rasimu ya Katiba mpya. Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na wenyeviti wa Kamati namba 10 na namba moja ya Bunge hilo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma kwa nyakati tofauti.

Akizungumzia juu ya mambo yaliyojiri, Mwenyekiti wa Kamati namba 10 wa Bunge hilo, Anna Abdalaah alisema kazi ya kuchambua Rasimu ya Katiba mpya inaendelea vizuri na wajumbe wengi wamependekeza mfumo wa Serikali mbili huku wakiwa na sababu zao ambazo zitaoneshwa katika ripoti watakayoitoa. Alisema Kamati yake ina wajumbe 52, ambapo upande wa Tanzania Bara una wajumbe 37 na Zanzibar 15.

“Hatuna matatizo ya kutoelewana, kazi inaenda vizuri leo tumemaliza masuala ya shirikisho na muungano, tumepiga kura hilo halitusumbui, hivi sasa tuko kwenye masuala ya ardhi,” alisema mama Anna.

Aliongeza kuwa katika kupitia vipengele vya rasimu hiyo yapo mambo ambayo wote wamekubaliana nayo mfano eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika ilikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari, ambapo wameongeza mito, maziwa, milima na anga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge hilo, Ummy Ali Mwalimu alisema katika suala la muundo wa Serikali wengi walitaka suala la Serikali Shirikishi liondolewe, huku wengi wakisema Ibara ibaki kama ilivyo.

Ummy aliongeza kuwa wanaendelea na mjadala hadi saa 2:00 usiku, hivyo kesho watapiga kura ili kuweza kumalizia vipengele vingine, hivyo Ijumaa hawataweza kuwasilisha ripoti yao na ameshamwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, kuhusu suala hilo. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, alisema bila kutaja upande upi alisema ukigawa upande mmoja katika 2/3 unapata 12 na mwingine saba, ambapo ikiongeza mtu mmoja unapata 2/3.

Naye Mwenyekiti wa Kamati namba moja Profesa Makame Mbarawa, Anna Kilango Malecela, ambaye Kamati yake ina wajumbe 53, Tanzania Bara 35 na Zanzibar 18 akizungumza kwa njia ya simu kwa waandishi wa habari, alisema wajumbe wote wanataka muungano, hivyo hakuna aliyesema hataki muungano.

Aidha Kilango alisema wapo baadhi ya wajumbe walitaka serikali mbili na wengine tatu, hivyo wamepisha kuhusu muundo wa Serikali uweje, hivyo wataendelea kupiga kura jioni.