Picha hii inaonyesha baadhi ya majengo Mtaa wa Samora yakibomolewa, ili kujenga mapya. Wenzetu nchi zilizoendelea wanayatunza na kuyaenzi majengo yao kama haya, kwani si sehemu ya historia na utamaduni wao. Kuyavunja majengo yetu tunayoyaita ya “zamani”, inaonyesha serikali yetu sio tu haithamini vilivyovyetu, bali haina mpango wowote madhubuti wa kulinda historia yetu kama mji na nchi kwa ujumla.
Ingekuwa vyema kama serikali yetu ingeyakarabati majengo kama haya, bila kupoteza miundo na uhalisia wake wa “zamani” . Bado tuna maeneo mengi ndani ya Tanzania hayajaendelezwa, sasa kwanini serikali isiende kujenga majengo yake mapya huko?
Picha na Mdau Chirwa