Baada ya Sare Kutawala EPL, Cheki Usajili Unavyofanyika Kwa Kasi

images-cms-image-000879690-1024x639Mohamed Elneny

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny. Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.
Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: “Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anafaa kucheza Jumapili.”
Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea msimu wa 2013-14.

Vidic_2815104b

Nemanja Vidic (34) mzaliwa wa Serbia ameamua kuingia makubaliano na klabu yake ya Inter Milan ili kuvunja mkataba wake kwa manufaa ya pande zote mbili.

Pamoja na kuichezea Inter mwaka mmoja na nusu, Vidic hakuwa na maisha mazuri kwa kuwa alianza kuichezea mechi yake ya kwanza akapata kadi nyekundu dhidi ya Torino pia majeraha yalikuwa yakimuandama sana na mwezi Agosti mwaka jana alipatwa na maumivu makali sana.

Pamoja na kutokuwa na maisha mema Inter msimu uliopita, Nemanja aliichezea timu hiyo mechi 23 na kuifungia bao moja.

Ezequiel_Lavezzi-2_3168571b

Baada ya kumtimua Jose Mourinho kocha aliyechukua mikoba hiyo, Guus Hiddink amekua akihaha kutafuta watu wa kuimarisha kikosi hicho ili kurudisha hadhi ya timu.

Katika mchakato huo Chelsea wameangukia kwa mshambuliaji wa PSG Ezequel Lavezzi mwenye umri wa miaka 30 raia wa Argentina.

Hata hivyo Chelsea itapata wakati mgumu kumpata mchezaji huyo aliyebakiza miezi 6 katika mkataba wake na kwa mujibu wa Allesandro Moggi ambaye ni wakala wake amesema Inter na Barcelona wanamtaka ila Inter ndo wameonyesha nia ya dhati.

joel-matip-hat

Katika kutaka kujiimarisha zaidi, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameamua kuanza biashara na Schalke 04 ya Ujerumani juu uwezekano wa kumpata Joel Matip.

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 anaweza kupatikana kirahisi kwavile katika mkataba wake amebakiza miezi 6 na hivyo kuwa rahisi kwa Schalke kumruhusu mcameroon huyo kwenda kwa majogoo hao wa Anfield.

shelveyceleb2_3183959b

Klabu ya soka ya Newcastle united imemsajili kiungo Jonjo Shelvey kutoka Swansea City.
Newcastle, wametumia kiasi cha pauni milioni 12 kumsajili kiungo huyu wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa 23.
katika vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu kukitumikia kikosi hicho cha Steve Mclaren.

Baada ya uhamisho huo kukamilika kocha mkuu wa kikosi cha Newcastle alimzungumzia mchezaji huyu na kusema “Ni mchezaji mwenye uzoefu katika viungo wa kati wa kiingereza.

Timu ya zamani ya Jonjo, Charlton,watapata kiasi cha mgao wa mchezaji huyo ambae alingara katika kiungo ya klabu ya Swansea msimu huu.