Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.
Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.
Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda kwa magoli 2-1 lakini jana ilijikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi.