Timu ya AZAM FC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Zesco United mchana wa jana leo katika mchezo wa michuano maalum katika Uwanja wa Levy Mwanawaswa mjini Ndola, Zambia.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye mvua kali, Zesco walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Jesse Were dakika ya kwanza tu.
Azam FC ilisota hadi mwishoni mwa kipindi cha pili ilipofanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 90.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Waziri Salum/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk67, David Mwantika, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao/Kipre Balou dk46, Frank Domayo, John Bocco/Allan Wanga dk67 na Kipre Tchetche