Azam FC ziarani Uganda, Rwanda

Nembo ya Timu ya Azam FC

TIMU ya Azam FC inatarajia kuondoka Jumatatu mchana na ndege ya Shirika la Ndege la Uganda kuelekea nchini Uganda na baadae Rwanda kukamilisha ziara yake ya maandalizi ya Ligi Kuu (VPL) inayotarajia kuanza August 20 mwaka huu.

Azam itaondoka baada ya kumaliza mchezo wa mechi ya kirafiki kati yake na timu ya Polisi Dodoma inayotarajia kufanyika Jumamosi ya Agosti 6, 2011.

Azam FC baada ya mchezo huo itaondoka Agosti 8 mwaka huu, kuelekea Uganda, na wakiwa huko watacheza mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu zinazoongoza katika Ligi Kuu ya nchini Uganda.

Kikosi kamili cha Azam kitawasili nchini jijini Kampala, Uganda siku hiyo hiyo na kucheza mchezo wake wa kwanza August 9 dhidi ya mabingwa wa ligi ya Uganda Bunamwanya FC mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Nakivubo.

Baada ya mechi hiyo siku inayofata timu itakuwa mapumziko na kufanya ziara katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchi Uganda (Tanzania High Commission). Agosti 11 Azam FC watacheza dhidi ya Sport Club Villa ya nchini humu na siku ya Ijumaa itacheza na KCC FC mechi zote zitachezwa katika uwanja wa Nakivubo.

Timu itapumzika siku moja kabla ya kucheza na Victors FC ambao ndiyo wenyeji wa Azam FC nchini Unganda siku ya Jumamosi ya tarehe 14 August, huo utakuwa mchezo wao wa mwisho kukamilisha ziara ya nchini Uganda, Azam FC itapumzika siku inaofata kwa maandalizi ya kuelekea nchini Rwanda Agesti 16, 2011 na kucheza na Polisi Rwanda Agosti 17, 2011.

Azam FC watarejea Tanzania Agosti 18, 2011 tayari kwa michezo yake ya Ligi Kuu ya Vodacom. Baada ya kukamilika ziara hiyo timu itarejea katika mazoezi ya siku mbili kwa ajili ya mechi ya yake ya kwanza ya ligi kuu ya Vodacom VPL, dhidi ya Moro United itakayofanyika Azam Stadium jijini Dar es Salaam.