Azam FC wawalalamikia waamuzi VPL

Kocha wa Azam FC (kushoto)

TIMU ya Soka ya Azam FC imelalamikia vitendo vya baadhi ya waamuzi wa Soka ndani ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, kwa kile kutoa upendeleo kwa baadhi ya timu. Kwa mujibu wa taarifa na mkanda wa video ambao Azam FC imeutoa kwenye mtandao wake, imeoneshwa kutoridhishwa na mwenendo wa waamuzi kwani wamekuwa wakikandamiza baadhi ya vilabu.
“Inawezekana Ngasa alikuwa offside lakini Bocco na Penati mbili je? dhuluma kama hizi pia zilifanywa Arusha dhidi ya JKT Oljoro na Tanga dhidi ya coastal Union. katika mechi zote tatu, Azam FC haikupoteza mchezo…” imesema taarifa ndani ya mtandao wa Azam FC.
Azam FC imetoa baadhi ya picha za mkanda wa video zikionesha magoli tata na matukio ambayo yanaonesha wazi kuwa na upendeo dhidi ya timu ambazo imekuwa ikipambana nazo.