Na Jaffer Idd
TIMU ya Azam FC Ijumaa inatarajia kwenda Tanga kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara Coast Union, mchezo unaotarajiwa kupigwa Ijumamosi katika uwanja wa Mkwakwani.
Azam inakwenda Tanga kwa mwaliko maalum wa timu ya Coast Union, ambayo inajiandaa kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kurejea tena katika mashindano hayo, ikiwa nje takribani miaka minne.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo katibu Mkuu wa Azam Nassor Idrisa ‘Father’ alisema wamepokea mwaliko wa mchezo mmoja dhidi ya Coast siku ya Jumamosi hivyo wapo katika maandalizi ya kuelekea uku ambapo timu itaondoka Ijumaa.
Idrisa alisema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, ukizingatia Tanga kwa Azam ni kama ipo nyumbani kwani imeshakitumia kituo cha Tanga katika Ligi msimu uliopita hivyo wanajisikia fahari kwenda tena Tanga kutoakana mapenzi ya masahabiki wa uko.
Alisema mchezo huo utakuwa ni changamoto kwa wachezaji wao wapya na wageni katika muendelezo wa kuunda kikosi cha kwanza cha timu hiyo, huku wakiendelea na mazoezi ya uwanjani pamoja na viungo GYM.
Katibu huyo alisema wanatarajia mchezo huo wa kirafiki utakuwa na upinzani kutokana na Coast msimu huu kusajili wachezaji wengi chipukizi na wenye uchungu wa soka na mkoa wao, ambapo alifafanua kuwa wasekia pia kuna wachezi wa kimataifa katika timu hiyo..
Idrsa alisema watakwenda Tanga na kikosi chao chote walichosajili msimu huu kasoro mchezaji Mrisho Ngassa aliyekwenda Marekani kwa majaribio kwenye timu ya Seatlle Sounders ambayo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu za Manchester United na Manichester City.
Akizungumza kutokea Tanga Katibu Mkuu wa timu ya Coast Unioni Salim Bawazir alisema kuwa, wanaisubiri Azam kwa hamu kubwa ili kukipa mazoezi na majaribio kikosi chao, baada ya kufanya mazoezi ya muda mrefu.
Bawazir alisema mpaka sasa timu yao ipo ziarani Mombasa ikijifua kwa mazoezi na mechi za kirafiki, ambapo inatarajiwa kutua Tanga Ijumaa ikitokea Mombasa , akizungumzia mchezo huo alisema mashabiki wa soka wa Tanga wanaisubili mechi hiyo kwa hamu kubwa ili kuangalia usajili wao walioufanya msimu huu.