Ayisha Nagudi kuiwakilisha Uganda Miss East Africa 2012

Miss Ayisha Nagudi mwenye urefu wa meta 1.82 ni mwanafunzi wa Mwaka II Chuo Kikuu cha Makelele jijini Kampala.

Na Mwandishi Wetu

MREMBO
aliyetangazwa mwishoni mwa wiki, Miss Ayisha Nagudi (23) kutoka nchini Uganda anatarajiwa kuiwakilisha nchi yake katika fainali za mashindano ya Urembo Afrika Mashariki na Kati (Miss East Africa 2012).

Washiriki wa kinyang’anyiro cha fainali za mashindano ya ‘Miss East Africa 2012’ wanaendelea kutangazwa katika mchujo ulioendeshwa na kampuni ya East Africa gazelle ya nchini humo.

Miss Ayisha Nagudi ana urefu wa meta 1.82 na Mwanafunzi wa Mwaka II katika Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala, ambapo anasomea Shahada ya Kwanza ya Ualimu (Degree ya Education).

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika September 07, 2012 jijini Dar es Salaam ambapo zitashirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.