Awamu Pili Shindano la SBL Kutafuta DJ Mbobezi Kuchanganya Muziki Yaanza

Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL, Stanley Samtu (katikati)  akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo alitangaza kuanza kwa msimu wa pili wa  shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.Kulia kwake ni Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija na kushoto ni DJ PQ ambaye ndiye Jaji Mkuu katika shindano hilo.

Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL, Stanley Samtu (katikati)  akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo alitangaza kuanza kwa msimu wa pili wa  shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.Kulia kwake ni Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija na kushoto ni DJ PQ ambaye ndiye Jaji Mkuu katika shindano hilo.

 

 

 

Meneja chapa wa vinwaji vikali Shomari Shija akifafanua jambo wkwa waaandishii wa habari katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za SBl Temeke jijini Dar es salaam,katikati ni jaji mkuu wa shindano hilo Dj PQ na kushoto mwishoni ni Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu .

 

 

Meneja Biashara wa SBL Esther Raphael akimkabidhi mmoja wa washindi waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la msimu wa pili wa  shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.

 

 

MaDJ waliofanikiwa kuingia msimu wa pili wa shindano la SBL la  kutafuta DJ mbobezi kuchanganya muziki wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

                                            ·        Kuibua vipaji vya ndani

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza  kuanza kwa awamu ya pili ya miezi mitatu ya shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutambulisha awamu ya pili  ya shindano hilo jijini Dar es Salaam  Mkuu wa Masoko na  Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu alisema kuwa shindano hilo  linadhaminiwa na kinywaji cha Smirnof Black Ice linamaanisha pia kuwapa wapenzi wa muziki kote nchini fursa ya kufurahia vibao vipya vya muziki vitakavyochezeshwa na ma+DJ  walio na vipaji katika sekta hiyo.
 “Leo tunatangaza ma+DJ 18 kati ya 40 kutoka mikoa mine  ambao wamefanikiwa  kuingia katika awamu ya  pili ambapo Dar es Salaam  wapo 10, Dodoma wawili, Arusha wawili, Morogoro wawili na Mwanza wawili,” alisema.
Kwa mujibu wa Samtu ni kwamba Smirnof Black Ice  ni chapa ya kinywaji inayoongoza  katika kipengele cha  kinywaji maarufu  miongoni mwa watumiaji wa tabaka la kati, katika maeneo yaote ya mijini na vijijini.
Tunaamini  kwamba kupitia shindano kupitia shindano hili SBL itatoa vipindi vya kufurahisha miongoni mwa wapenzi wa muziki watakaotembelea  yatakakofanyika mashindano na wakati huo huo kuwapatia fursa ya kipekee  ya kuibua, kukuza na kuangalia vipaji vilivyopo katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.”
 Alisema kwamba kundi  la  vipaji vinavyosakwa katika mashindano hayo ni la vijana walio na umri kati ya  miaka 18 hadi 30, ambao kwa mujibu wa Samtu  ni kwamba shindano hilo linawafaa wanafunzi  walio katika ngazi ya eilimu ya juu  pamoja na wanataaluma ambao ni vijana. vijina.
“Zitatolewa zawadi nzuri kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kudokeza  kuwa zawadi hizo ni pamoja na seti ya  vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato, na mashine ya kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakafika fainali.
  
“Tunatoa wito kwa  kwa ma-DJ wote , wasimamizi wa mabaa na wapenzi wa muziki katika miji hii  kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili waweze kuifurahia sekta ya muziki ya Tanzania,” alisema Samtu.