Askofu Kakobe Ampa Mtihani Rais Kikwete Mkutanoni

IMG_0283

Mkutano wa pamoja wa vyama vya CUF,  CHADEMA na NCCR-Mageuzi Ukiendelea.

IMG_0383

Viongozi wakuu wa vyama hivyo,  yaani James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe  (Mwenyekiti Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti CUF) wakiwa kwenye mkutano huo.

IMG_0278

IMG_0284

IMG_0308

IMG_0315

IMG_0329

IMG_0341

 

Wananchi, wanachama na wapenzi wa vyama hivyo wakiwa kwenye mkutano na mabango anuai.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia
Kakobe leo ameibukia katika mkutano wa pamoja wa vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi na kutoa kauli aliyoiita ni mtihani kwa Rais Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama wa vyama hivyo na wananchi, Askofu Kakobe akisalimia umati huo amemtaka Rais Kikwete kutotia saini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 ambao umezua mgogoro.

Akifafanua Askofu Kakobe alisema huu ni mtihani mwingine wa rais Kikwete na ataufaulu endapo atagoma kutia saini muswada huo ambao ulizua vurugu bungeni kati ya vyama vya upinzani vinaodai maoni ya wananchi na vyama vya siasa yamechakachuliwa.

Alisema Rais Kikwete alionesha msimamo wa dhati tangu awali kwa kuidhinisha hoja ya kuanza kwa mchakato wa uundaji katiba mpya licha ya kupingwa na baadhi ya wana CCM ndani ya chama hicho.

“…Wakati zoezi hili (mchakato wa katiba mpya) linaanza chama tawala CCM ilikataa kata kata pamoja na Serikali yake katiba isibadilishwe, Waziri wa Katiba na Sheria na kila mtu aliyezungumza alikataa, ni Jakaya Mrisho Kikwete peke yake alipiga kifua akasema hapana tufanye zoezi hili tupate katiba mpya, tena minong’ono mingi
ilikwenda kinyume nae…chokochoko chungunzima zikawepo kumshambulia kwamba alifanya makosa…” alisema Askofu Kakobe.

“…Sasa hapa ndipo kwenye mtihani mwingine wa Jakaya Mrisho Kikwete…ulianza vizuri Jakaya Mrisho Kikwete ukaenda kinyume hata na wana CCM wenzako kwa kuwa ulikuwa na mapenzi mema na nchi yetu, sasa huu ni mtihani mwingine ukisaini muswada huu umeshindwa mtihani…angalia umati wote huu upo kinyume na mswada huo ukisaini
tutaamini kuwa tangu mwanzo ilikuwa danganya toto..,” alisema Kakobe.

Mkutano huo Mkubwa ulihutubiwa na viongozi wakuu wa vyama hivyo, yaani James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF).

Akizungumza katika mkutano huo, Mbatia alisema kitendo cha wabunge wa CCM kuupitisha muswada huo kibabe pasipo busara ni kuzua mgogoro wa kikatiba jambo ambalo lihatari kwa taifa. Alisema vyama vya siasa pamoja na wananchi hawatakubali hali hiyo na nilazima ipatikane Katiba Mpya kwa gharama yoyote ile.

Alisema katiba inayoandaliwa kwa sasa ni ya matumizi ya miaka mingi na si kuangalia leo tu, hivyo kuna kila sababu ya kuridhiana na kushirikishana kwa kila mmoja na si upande mmoja kujitwalia mambo utakavyo kama ilivyo sasa. Alishauri wadau wote wanaoguswa kukaa katika meza za majadiliano ili ku.

Akizungumza na umati wa wananchi Mbowe alisema taifa haliwezi kupata katiba mpya endapo wananchi wataendelea kuwa waoga na wenye hofu; “katiba si suala la kisiasa pekee bali la wananchi wote hivyo haina budi kushirikiana kwa pamoja.”

Mbowe alisema viongozi wa vyama vya siasa wataendelea kuzungumza na wadau mbalimbali wanaoguswa na suala la katiba wakiwemo viongozi wa dini na makundi mbalimbali kukutana na kuangalia nini cha kufanya kufikia muafaka kutetea mchakato wa katiba.

“Kwa sheria iliyopitiswa na Kama sheria hii haikurekebiswa hatuta shiriki mchakato wa katiba, kuanzia bunge la katiba Tutatumia mbinu mbalimbali zinazokubalika ulimwenguni kupaza sauti zetu kupinga mchakato wa katiba wa Tanzania kwamba ni mchakato usioshirikishi kwa wananchi wake.”

“Maandamano ni haki ya kikatiba hivyo kwa sasa yatafanyika Oktoba 10, 2013 siku ya Alhamisi hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kudai haki yao. “…Siku hiyo itakuwa maalumu ya kudai haki ya katiba mpya..hatuwezi kwenda kumuomba Rais Kikwete ikulu tuzungumze na kunywa chai wala juisi.”

“Maandamano yatafanyika nchi nzima ikiwa ni kupinga mchakato wa katiba kuhodhiwa na chama kimoja, vyama vyetu vitaendelea kuratibu maandamano na utaratibu wa mikutano kupinga udhalimu huo.” alisema Kiongozi huyo.