Na woinde shizza, Arusha
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja amewataka Watanzania
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo ya taifa.
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo ya taifa.
Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo
itakayoleta mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.
itakayoleta mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.
Akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji
Viongozi waadilifu na wenye bidii.
Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza taifa hili” Alisema Isanja
Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni wa heshima katika
mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa
misingi ya ukabila na udini na kutowachagua kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.
mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa
misingi ya ukabila na udini na kutowachagua kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.
Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa
tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na linategemewa kukamilika nchini kote ili kukamilisha uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza
tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.
tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.