Askari wa Operesheni Saka Majangili Walalamikiwa Kuchoma Nyumba za Wanakijiji Kabage, Mpanda

Wanakijiji wakikihama kijiji chao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na timu ya wanaoendesha operesheni saka majangili.

Wanakijiji wakikihama kijiji chao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na timu ya wanaoendesha operesheni saka majangili.

Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku

Hizi ndizo nyumba zao, wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na kusababisha maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti.

Mzee na binti yake wakiwa wanaondoka wanaondoka.

Wakina mama wakiwa wanafungasha

Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho

Wakiendelea kuhama kijijini hapo


Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba KT/KIJ/47.

Hawana makazi tena hawa

Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto

Mchungaji wa kanisa la PAG wa Kijiji cha Mwamkulu Petro Mahenga akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba zao katika kijiji cha kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari  hao hata hivyo mtoto huyo aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa

Dogo akiwa ameishiwa Nguvu

 Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa.

Na Walter Mguluchuma-Kativi yetu Mpanda
ASKARI waliokuwa wanafanya operesheni ya kuwasaka majangili waliokuwa wakiongozwa na JWTZ  wamelalamikiwa kwa kuchoma nyumba za wanakijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na
kuwasababishia wananchi wa kijiji hicho kuishi chini ya miti na akina mama kujifungua kabla ya wakati.
 
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Maganga Kasope alisema tukio hilo lilitokea hapo Oktoba 28 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na kusababisha zaidi ya kaya mia sita kukosa makazi ya kuishi. Alisema kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu kumi ni kijiji halali kwani kalisajiliwa  toka mwaka jana na kupewa usajiri wenye namba za usajiri wa kijiji KT/KIJ/47 hivyo wameshangazwa na wakazi wa kijiji hicho kuchomewa nyumba zao wakati ni kijiji halali.
 
Alisema kuwa katika tukio hilo akina mama watatu ambao walikua wajawazito walilazimika kujifungulia kwenye mbuga za mpunga wakati wakikimbia kuelekea kijiji cha jirani cha mwamkulu kujihifadhi hivyo kutokana kutembea kwa umbali mrefu hivyo ililazimika kujifungulia njiani na kujifungua watoto wakiwa salama.
Kwa upande wake mhanga wa tukio hilo  Daudi  Lulehiwa 28  alisema kutokana na tukio hilo iliwalazimu ketembea umbali mrefu kwa ajiri ya kukimbilia katika kijiji cha jirani cha Mwamkulu huku wakiwa wamebeba mizigo yao na iliwalaziri hata watoto wao wadogo kutembea kwa miguu umbali huo mrefu.
 
Alisema mkewe aitwaye Kulwa Elias 24 ambae alikuwa ni mjamzito wa miezi minane kutokana na kutembea umbali huu huku akiwa amebeba mizigo  aliweza kujifungua mtoto wa wakike  ambae alikuwa sio
ridhiki na alifariki muda mfupi baada ya kujifungulia chini ya mti.
 
Naye Mchungaji wa Kanisa la wa Kanisa la P.A.G wa Kijiji cha Mwamkulu Mchungaji Petro Mahega  alisema toka wahanga hao waliokimbilia kijijini hapo wamekuwa wakiishi kama wanyama wao na familia zao. Alieleza kutokana na wahanga hao kuishi chini ya miti na mbaya zaidi hapo juzi walinyeshewa na mvua ambayo ilinyesha majira ya usiku hivyo ametowa jengo la Kanisa lake igawa ni dogo sana litumike kwa ajiri ya kuwahifadhi wahanga hao.
Kwa upande wake mhanga mwingine Malidadi Gwachele 72 ambae anaishi na familia yake ya watu 20 wakiwa chini ya mtu alieleza kuwa  wameanza kuhathirika kwa kupata magonjwa ya kuharisha.
 
Alisema hari hiyo imesababishwa na maji wanayo kunywa na mazingira wanayoishi na hasa watoto wadogo ndio wanao athirika zaidi na magonjwa hayo. Kwa upande wake, Mdae Masanja  alisema mbali ya kuchomewa nyumba yake pia amepoteza chakula chake ambacho kiliteketea kwa moto baada ya kushindwa kukihamisha kwenye  nyumba yake wakati ikiungua.
 
Alisema sasa hivi wanalala nje bila hata kujali jinsia za familia walizo nazo kutokana natukio lenyewe inawalazimu walale hivyo na wamekuwa wakijisaidia kwenye vichaka. Aidha Mhanga Katali Ngeleja  alieleza mbele ya mwandishi wa habari hizi ambae alitembelea eneo hilo kuwa wako watoto wenye umri
kati ya miaka saba na nane  walipotezana na familia zao kwa muda wa siku mbili.
 
Alieleza yupo pia mwenzao mmoja ambae alikuwa anamiliki mashine ya kusanga unga iliteketea kabisa kwa moto ikiwa ndani ya kibanda cha nyumba.