Askari wa JWTZ Brian Salvatory Rweyemamu Kuzikwa Leo Dar

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian anatarajiwa kuzikwa kesho mchana(Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Rais Dk. Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Private Brian Salva Rweyemamu aliyefariki dunia Mei 15, 2014 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu anatarajiwa kuzikwa leo. Marehemu Private Brian Rweyemamu ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu atazikwa katika makaburi ya Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam mchana. Ufuatao ni wasifu wa marehemu pamoja na ratiba ya mazishi yake;

WASIFU WA PRIVATE  BRIAN SALVA RWEYEMAMU

Rwechungura Brian Salvatory Rweyemamu, aliyefariki dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.

Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar es Salaam kabla ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.

Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni, Dar Es Salaam, mwaka 1998.

Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999, ambako alikaa miaka minne kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.

Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.

Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.

Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe 10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza fahamu.

Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano.

RATIBA YA MAZISHI YA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU, NA WASIFU WAKE

MAZISHI LEO JUMAMOSI TAREHE 17.05.2014 

SHUGHULI ZOTE ZITAFANYIKA NYUMBANI KWA BW. SALVA RWEYEMAMU KINONDONI, MKABALA NA VIJANA HOSTEL NA MANGO GARDEN, JIJINI DAR ES SALAAM

SAA  1.00:  ASUBUHI KIFUNGUA KINYWA – NYUMBANI

SAA 4.00-5.00:  CHAKULA CHA MCHANA – NYUMBANI

SAA 5.00-6.00: KUAGA MWILI – NYUMBANI

SAA 6.00-7.00: MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA

SAA  8.00 Mchana: SHUGHULI ZA MAZISHI MAKABURI YA KINONDONI