Asilimia 38 ya ‘Walevi’ Kinondoni Walianza Utotoni

Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.

Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo (katikati) akionesha ripoti ya utafiti juu ya matumizi ya pombe na inavyochangia unyanyasaji wa kijinsia kwa Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT ambalo ndio wawezeshaji wa utafiti huo. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT. Ripoti hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.

ASILIMIA 38 ya wanywaji wa pombe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaa walianza matumizi ya pombe wakiwa watoto. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT imebainika kuwa asilimia 26.5 ya watumiaji pombe walianza wakiwa watoto yaani kati ya umri wa miaka 14 hadi 17, huku asilimia 11.8 walianza matumizi ya pombe wakiwa chini ya miaka 14.

Akisoma matokeo ya hayo leo jijini Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa Utafiti huo, Dk Severine Kessy alisema utafiti huo umefanyika mwezi Juni, 2014 na uliendeshwa katika Kata Tatu za Wilaya ya Kinondoni yaani Kata ya Makumbushi, Kata ya Wazo pamoja na Kata ya Saranga iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaa.

Dk. Kessy alisema utafiti huo ulioendeshwa kwa njia ya mahojiano kwa baadhi ya wananchi, majadiliano kwenye vikundi mbalimbali, mahojiano kwa baadhi ya viongozi wa Kata, mitaa na viongozi wa baadhi ya taasisi ulibaini pia idadi kubwa ya watumiaji pombe ni wasomi wenye elimu za vyuo ikilinganishwa na wasioenda shule.

Alisema takwimu za utafiti zimebaini kuwa asilimia 80 ya wananchi wenye elimu ya vyuo walikubali wanatumia pombe, huku ikibainika asilimia 55 ya wananchi wenye elimu ya ya kidato cha sita wanatumia pombe na ni asilimia 50 tu ya wananchi wasiokwenda shule ambao wamekiri wanatumia pombe.

Asilimia 55.5 ya wanaume waliohojiwa katika utafiti huo wamekubali wanaitumia pombe na ni asilimia 44.5 ndio walikataa kutumia pombe. “…Kwa upande wa wanawake asilimia 40.3 walikubali kutumia pombe huku asilimia 59.7 wakionekana kukataa kuitumia pombe.”

Alisema utafiti huo pia umebainisha asilimia 39 ya wananchi waliohojiwa walikiri wamejikuta wakinywa pombe bila kushawishiwa na yeyote, huku asilimia 38 wakiweka wazi kuwa wamejikuta katika matumizi ya pombe baada ya kushawishiwa na marafiki zao. Alisema utafiti huo pia ulibaini kuwa asilimia 13 ya waliokubali wanatumia pombe walikiri kwamba wameshawishiwa na wazazi wao nyumbani.

Akizungumzia kiwango cha unywaji pombe kwa watu waliokiri kutumia pombe, alisema asilimia 31 walisema hutumia zaidi ya chupa tano kwa kila wanapoanza kunywa huku asilimia 26 wakitumia kati ya 3 hadi nne kwa kila wanapokunywa pombe.

Alisema asilimia 63 ya waliohijiwa walisema wamezungukwa na sehemu nyingi za kuuzia bidhaa hiyo tena kwenye makazi ya watu, huku sehemu nyingine zinazofanya biashara hizo kwa wingi hazipo rasmi licha ya kuendelea kufanya biashara hizo.

Alisema utafiti huo pia ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanyaji wanajua madhara ya pombe kiafya lakini bado wanaendelea kunywa, huku wakiziomba mamlaka zinazohusika kuwasaidia kuweka utaratibu utakaopunguza matumizi ya pombe kutumikia.

“…Asilimia 48 ya wanywaji walishauri kuna haja ya kuwa na sheria kali itakayopunguza matumizi ya pombe kupindukia, huku pombe ikionekana kuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la watoto wa mitaani,” alisema Dk. Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

Alisema madhara makubwa ya unywaji wa pombe katika utafiti huo yameonesha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili pamoja na watoto wa mitaani, kwani idadi kubwa ya walivi wameonekana wapo waliotelekeza au kushindwa kuzihudumia familia na hivyo watoto kutangatanga hovyo mitaani.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo alisema idadi kubwa ya malalamiko wanayopokea katika kituo chao cha ushauri na msaada wa kisheria kwa jamii unywaji wa pombe kupindukia unachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vipigo kwa akinamama na utelekezaji familia kwa wanywaji.