Ashikiriwa na Polisi baada ya kumnajisi mbwa

mnym nyependw nyubni

Na mwandishi wetu Kilimanjaro

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maganga Patrick (30)mkazi wa Uru Mwas wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na Mbwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw. Robert Boaz alisema mtu huyo alikamatwa Juni Nane majira ya saa nne usiku katika eneo la Uru Mwas nyumbani kwa Bw. Felex Lyimo ambaye ni tajiri yake.

Kamanda Boaz alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa Bw. Felex Lyimo siku ya tukio alifumaniwa na taajiri yake huyo na kwamba mbwa aliyekuwa akifanya naye mapenzi ni wa nyumbani humo.

Aidha kamanda alisema uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kumpima mtuhumiwa akili ili kujua kama ana akili timamu na pindi upelelezi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.

Katika tukio jingine watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kukutwa na katoni 62 zenye viroba 8,928 vya pombe bandia aina ya Konyagi.

Kamanda Boaz alithibitisha kukamatwa kwa watu hao juni Nane majira ya saa tano usiku eneo la barabara ya Kibosho wilaya ya Moshi kufuatia operesheni inayofanywa na jeshi hilo katika mkoa wa Kilimanjaro.

Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Neema Philipo (20) mkazi wa katanini Karanga,Deogratius Kway (21) pamoja na Clemence Adolph (20) ambapo walikutwa nyumbani kwa Bi. Neema Philipo wakiwa na pombe hiyo ya bandia.

“Watu hawa wanatengeneza pombe mwitu na kuifunga kwenye vipakti vya konyagi vijulikanavyo kama virob lakini hii si konyagi ni bandia”alisema Kamanda Boaz.

Alisema kwa sasa uchunguzi zaidi unaendelea na ukikamilika watafikihwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Tukio hilo limetokea ikiwa zimepita siku chache toka kamati ya ushauri ya mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kutaka pombe ya konyagi ifuatiliwe kwa madai kuwa inawharibu vijana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Katika kikao hicho ilielezwa kuwa kumekuwepo na konyagi(viroba) bandia ambavyo vinatokana na pombe haramu aina ya gongo iliyowekwa kwenye vipakti ya viroba jambo amblo ni hatari kwa ustawi wa nchi.

Wakati huohuo mwanafunzi wa chuo cha KCMC aliyejulikana kwa jina la Upendo Aberd (47) anashikiliwa na jeshi lapolisi mkoani hapa kwa thuma za kukutwa na noti bandia tano za sh. 10,000.

Kamanda Boaz alisema mama huyo alikamatwa juni nane majira ya saa 12 jioni eneo la KCMC Mapipa manispaa ya Moshi mkoani hapa na kwamba fedha hizo tatu zilikuwa na Na. BF 1547947, Na. BF 1547948 na nyingine Na. BC 2937331.