TIMU ya Ashanti United Ilala ya Dar es Salaam jana iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Tesema ya Temeke bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliochezwa uwanja wa Mabatini Mkoa wa Pwani. Ashanti ambayo ipo kundi B imefikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi nne inashikilia usukani kwenye kundi hilo.
Bao la Ashanti lilifungwa kipindi cha kwanza dakika ya 38 na Abdul Mwarami. Timu ya Ashanti kwa sasa inajipanga kuhakikisha inarudi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutokana na uwezo unaooneshwa wawapo uwanjani na katika mechi zake zote alizoshiliki Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Polisi Dar es Salaam iliifunnga Ndanda ya Mtwara mabao 4-0.
Mabao ya Polisi yalifungwa na Magige Belence dakika ya nne, Henrinco Kayombo dakika ya 51, Patrick Mrope dakika ya 60 na Arnoor Salim dakika ya 83. Kundi C ulichezwa mchezo mmoja kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora ambapo wenyeji Rhino waliifunga Mwadui ya Shinyanga mabao 2-0. Mabao ya Rhino, mmoja lilitokana na beki wa Mwadui Lulanga Mapunda kujifunga dakika ya 18 na la pili lilifungwa na Victor Hagaya dakika ya 86.
Mjini Morogoro, uwanja wa Jamhuri uliochezwa mchezo mmoja kati ya Burkina Faso na Small Kids na walitoka suluhu ya 0-0. Mchezo huu ulikuwa kiporo baada ya kuahirishwa kutokana na Small Kids kuchelewa kufika Morogoro kwasababu gari lao liliharibika.