Na Joachim Mushi
MKURUGENZI wa Asasi za Kiraia nchini (The Foundation for Civil Society), John Ulanga amesema utaratibu wa kutoa tuzo kwa asasi za kiraia zinazofanya vizuri zaidi katika utekelezaji miradi yao umechochea uwajibikaji na utendaji kwa asasi nyingi.
Ulanga alitoa kauli hiyo jana usiku jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuzizawadia asasi za kiraia zilizofanya vizuri kwa utekelezaji wa miradi yao anuai kwa jamii, hafla iliyoandaliwa na taasisi hiyo ya kijamii.
aidha Ulanga alisema utaratibu huo wa kuzikumbuka kwa tuzo asasi na wanaharakati waliochangia shughuli hizo ulioanza kutekelezwa mwaka 2008 umeleta mabadiliko makubwa kwa hasa ufanisi katika utekelezaji wa miradi kutokana na ushindani.
Alisema miongoni mwa vipengele vilivyozingatiwa katika utoaji wa zawadi hizo ni pamoja na Ushiriki Sera, Utawala Bora, Uwajibikaji na Asasi iliyojenga uwezo na Ukuzaji wa Mitandao.
Asasi mbalimbali zilizofanya vizuri zaidi zimejinyakulia zawadi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo na wanaharakati wa masuala ya kijamii.
Asasi ya Saidia Wazee Karagwe imetwaa ushindi wa jumla katika tuzo hizo. Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya hafla hiyo;-