Asasi za Kiraia na Taasisi Binafsi Zatakiwa Kuwa Wazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (wa kwanza kulia).

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika utakavyoleta maendeleo katika nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.

Angelina Misso (katikati) akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (kulia) namna Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT) kinavyofanya kazi na sekta mbalimbali katika matumizi sahihi ya takwimu huria mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Biasha Mkenga kutoka Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT), Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Baadhi wa Makatibu Wakuu na Manibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akiongea na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika jijini Dar es Salaam.

Na Beatrice Lyimo, Maelezo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amawaasa Asasi za kiraia na Taasisi binafsi kuwa wazi katika masuala yao katika shughulizao kwa wananchi ili kuleta maendeleo nchini. Rais Kiwete amesema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais Kiwete amesema kuwa mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika ni wa kwanza na wa aina yake kufanyika Barani Afrika na Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji ambapo imeshirikiana na Benki ya Dunia katika kuandaa mkutano huo.

Dk. Kikwete ameongeza kuwa heshima hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) unaolenga kuifanya Serikali kuwa wazi na hivyo kuleta uadilifu na uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi.

“Katika utekelezaji wa Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika kuanzisha Tovuti ya Takwimu Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za Serikali na Taasisi zaka,” amefafanua Rais Kikwete.
Naye Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta maendeleo hususani kwa nchi za Afrika ikiwemo mwenyeji Tanzania.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Takwimu huria itawasaidia wananchi kujua nini kinaendelea katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji, elimu na afya ambazo ndio sekta zinazogusa jamii kwa ukaribu na kupelekea kuanza na sekta hizo. Pia ameongeza kuwa sera ya Takwimu huria ipo kwenye matayarisho na inategemewa kuanza kutumika baada ya miezi sita ijayo na hivyo kumfanya mwanachi kuweza kuingia kwenye mtandao na kujua matatizo yanayoikabili jamii.

Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wea mkutano huo amesisitiza kuwa nchi za Afrika zitumie takwimu huria kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi zao kwani zinasaidia kupata fursa mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa ajira na pia kumfanya mwananchi kufanya uchambuzi wa kutosha kwa kufuata viwango na kujua hali halisi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi taifa yao.

Mkutano huo unaoendelea jijini Dar es salaam unajumuisha takribani nchi 30 kutoka ndani na nje ya Afrika kwa kushirikisha wawakilishi mbalimbali kuwakilisha Serikali zao, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na Washirika mbalimbali wa Maendeleo.