Asasi ya Marafiki Charity Tanzania Wafuturisha Watoto Yatima Dar

Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY,

ASASI isiyo ya Kiserikali ya Marafiki Charity Tanzania ‘Marafiki Charity’, kwa umoja wao jioni ya jana Juni 24. 2017, wameweza kujumuika kwa pamoja katika tukio maalum la kufuturisha katika kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA. Marafiki hao waliweza kuandaa futari hiyo maalum na kwenda kujuika pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha CHAKUWAMA, chenye makazi yake Sinza-Mori (CHAKUWAMA). Aidha wakitoa shukrani kwa niaba ya Asasi hiyo ya Marafiki Emmanuel Makundi na Omary Mkambara walieleza kuwa, moja ya shughuli waliokuwa wamepanga ni kufanikisha tukio hilo la kujumuika pamoja na watoto hao ikiwa ni njia moja wapo ya kutoa sadaka jamii yenye uhitaji.

“Tumeweza kujumuika hapa kwa pamoja tukiwa Marafiki. Hii ni moja ya kuonesha upendo, undugu, uelewano na hutu wetu kwa wenzetu wa kituo hichi cha CHAKUWAMA.” Alieleza Makundi.

Kwa upande wake, Omari Mkambara alieleza kuwa, huo ni mwanzo kwani wamefurahia uwepo wao hapo wa kupata kufuturu pamoja hivyo ikiemo dua walioombewa ni faraja kwa umoja wao huo. Marafiki Charity ni muunganiko wa marafiki kutoka kada mbalimbali, waandishi wa Habari, wanasheria, wahandisi, wajasiriamali, wahasibu na watu mbalimbali ambapo wanashirikiana na kwa pamoja katika kusaidia jamii ikiwemo kufanya kazi kwa pamoja za kujitolea, kusaidia wasiojiweza, kubadilishana mawazo na kujumuika pamoja katika mustakabali wa kuijenga Tanzania.

 

Vijana wa Marafiki Charity wakipeana majukumu kabla ya kuanza jukumu la kufuturisha watoto hao wa CHAKUWAMA.

Ebby mwenye jezi nyeusi akiwatambulisha baadhi ya vijana wenzake wa Marafiki Charity kwa mmoja wa walezi wa kituo cha CHAKUWAMA wakati walipowasili hapo jana Juni 24.2017 katika tukio hilo la kuwafuturisha watoto hao wanaolelewa kituoni hapo.

Baadhi ya wanaumoja wa Marafiki Charity wakiwa kwenye pozi tofauti, akiwemo Devotha, Leah Mushi aliyembeba mtoto Malaika Ebby, Munira Hussen, Esther Namuhisa na Pendo.

Omary Mkambara akijadiliana jambo na Naamala katika tukio hilo la kufuturisha

Wakibadilishana mawazo wakati wakisubiria muda

Omary Mkambara akiwajibika katika tukio hilo

Wakisaidia kushusha futari maalum

Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY.

Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY.

Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY.

Shughuli ya futari ikiendelea

Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiendelea kujumuika pamoja katika furai hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY

zoezi la futari likiendelea

Marafiki Charity wakijumuika pamoja katika kupata futari hiyo

Omari Mkambara na Emmanuel Makundi (kulia) wakitoa neno la shukrani kwa kituo hicho

Omary Mkambara akitoa neno la shukrani

Dua maalum kwa ajili ya tukio hilo

Mmoja wa wasimamizi katika kituo hicho akiwatambulisha Marafiki Charity kwa Mama mwanzilishi wa kituo hicho


Marafiki Charity wakimsikiliza Mama Mwanzilishi wa kituo hicho wakati walipofika kumjulia hali

 

Mama Mwanzilishi wa kituo cha CHAKUWAMA akiwaombea dua Marafiki Charity


Baadhi ya Marafiki Charity wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza tukio la kufuturisha watoto wa kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA, tukio hilo limefanyika jana Juni 24.2017.