Arusha Yachaguliwa Kujiunga Mtandao wa Miji 100 ya Kustawi Kiuchumi

Sehemu ya Mji wa Arusha Tanzania (Uhuru Monument)

Sehemu ya Mji wa Arusha Tanzania (Uhuru Monument)


 
MJI wa Arusha umechaguliwa pamoja na miji mingine 32 kujiunga na mtandao wa miji 100 ya kustawi kiuchumi. Tangazo hilo limetolewa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Taasisi ya Rockefeller Foundation mjini Singapore.
 
Hili wimbi la pili la majiji litaungana na majiji 32 ambayo yalishinda Changamoto ya Majiji 100 yaliyoweza kustawi tena kiuchumi mwaka jana na kutengeneza mtandao unaokua wa maeneo ya mijini duniani kote kwamba iko tayari kukabiliana majanga ya kijamii, kiuchumi na kimwili na misongo ya mawazo ambayo ni sehemu inayoongezeka ya karne ya 21.
 
Mji wa Arusha ni aa mji mkubwa ya kiuchumi hapa Tanzania na pia ni kitovu cha diplomasia katika jumuiya ya Afrika mashariki. Changamaoto zamjii huu ni pamoja na kuzeeka kwa miundombinu, ukame, mafuriko, uhaba mkubwa wa ajira na ugaidi.
 
Ukuaji uchumi mijini ni uwezo wa watu binafsi, jamii, taasisi, biashara na mifumo ya kuishi, kuiga na kukua bila kujali ni aina gani ya matatizo sugu na mishituko mikubwa wanayopata. Kutoka madhara ya tufani kubwa mpaka kuongezeka kwa kutokuwepo usawa wa kijamii na kiuchumi au uwezo wa mifumo ya majiji kuweza kukabiliana na ongezeko la watu na upungufu wa usambazaji chakula, majiji 100 yaliyoweza kuibuka tena kiuchumi inalenga kuipa maeneo ya mijini zana na kusaidia mtandao kubuni, kuendeleza na kutekeleza kiujumla ufumbuzi.
 
“Kila jiji ni la kipekee, na kupitia mtandao wa 100RC, majiji yanakuwa kwa kutegemeana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kuibuka tena kiuchumi,” alisema Michael Berkowitz, rais wa majiji 100 yaliweza kuibuka tena kiuchumi.
 
“Kwa kuunganisha majiji kwa majiji na wataalamu wa ujenzi wa kuibuka tena kiuchumi, sisi tunalenga kujenga muundo wa kimataifa wa ufumbuzi wa kuibuka tena kiuchumi ili majiji yaweze kukabiliana na changamoto za karne hii ya mijini kwa ufanisi zaidi,” Berkowitz.
 
“Wanachama wa mtandao wa majiji 100 yaliyoweza kuibuka tena kiuchumi kwa haraka wanaongoza duniani katika kuonesha kwamba si tu inawezekana kukua tena kiuchumi mijini katika kila aina ya jiji, lakini ni muhimu,” alisema Dk. Judith Rodin, Rais wa taasisi ya Rockefeller Foundation.
 
“Majiji yanakujifunza kwamba kwa kujenga ukuaji tena kiuchumi, si tu wao kuwa bora tayari kwa ajili ya nyakati mbaya, lakini pia maisha ni bora katika nyakatinzuri, hasa kwa watu maskini na wanaoweza kukubwa na mazingira magumu. Ni uwekezaji mzuri, na hutoa gawio la kuibuka tena kiuchumi ambao ni ushindi kwa kila mtu. ”
 
Sehemu ya Mji wa Arusha Tanzania

Sehemu ya Mji wa Arusha Tanzania

Huku idadi ya watuwanaoishi maeneo ya mijini ikikua kutoka asilimia 50 ya idadi ya watu duniani hadi takribani asilimia 70 kwa mwaka 2050, majiji duniani kote lazimayakubali athari za ukuaji haraka wa majiji, utandawazi, tabia nchi, na majanga ya asili na yale yanayosababishwa na binadamu.
 
Kujenga Mtandao wa Miji inayostawi tena kiuchumi duniani
 
Orodha hiyo yenye mambo mbalimbali inaonesha haja ya kujifunza kutoka katika majiji ya ukubwa wowote duniani kote ili kunakili na kubuni. Majiji katika mtandao wa majiji 100 yaliyoweza kuibuka tena kiuchumi yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimazingira na kijamii – kuanzia vitisho vya mafuriko na hali mbaya ya hewa, kwa kuongeza matatizo katika miundombinu na afya, na kuongezeka matatizo ya kiuchumi – na yapo katika viwango tofauti vya safari yao kuelekea kujenga majiji yaliyostawi kiuchumi.
 
Kila jiji kwenye mtandao una haki ya kupokea fedha za ruzuku kwa kuajiri Ofisa Mkuu wa Ustahimilivu ambaye ataongoza uchambuzi, upangaji na utekelezaji wa mkakati wa uvumilivu wa jiji hilo, kufanya kazi na mashirika mbalimbali ya serikali na katika sekta ya jamii.
 
Pia yatapokea msaada wa kiufundi na huduma wanazohitaji huku wakifanya kazi kuelekea kutekeleza mkakati huo na pamoja na upatikanaji wa aina mbalimbali ya washirika katika sekta binafsi na umma, na sekta zisizo na faida. Washirika hawa watatoa zana katika maeneo kama vile ubunifu wa kifedha, teknolojia, miundombinu, matumizi ya ardhi, na ustawi kijamii.
 
Mchakato wa Uchaguzi
Kasi kutoka changamoto ya kiuzinduzi mwaka jana iliufanya mwaka huu kuwa wa ushindani mkubwa, kwa zaidi ya nchi 90 katika mabara sita. Majiji ya mwaka huu yalichaguliwa kutoka karibu waombaji 350 kwa misingi ya uwezo wao wa kuonyesha maono ya kipekee ya kustawi tena kiuchumi, uwajibikaji wa muda mrefu kwa kupitia maghala ya serikali nasekta ya jamii, kipaumbele kikiwa mahitaji ya watu maskini na wanaoishi katika mazingira magumu. Majiji ya kimtandao yanakuwa kama mfano wa kuigwa na majiji mengine duniani ambayo yanataka kujijenga kiuchumi.
 
Majiji wanachama yalichaguliwa kwa mapendekezo ya jopo la majaji wa kimataifa, wakiwemo rais wa zamani José María Figueres Olsen wa Costa Rica; Dk. Donald Kaberuka, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika; Dr. Isher Ahluwali, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana katika Baraza la India kwa ajili ya Utafiti kuhusu Uhusiano wa Kimataifa wa Uchumi, na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Asia, Josette Sheeran. Changamoto kwa majiji 100 yaliyoweza kustawi tena kikuchumi ni kufungua mzunguko wake mwingine wa maombi ya majiji katikati ya mwaka 2015.
 
Miji iliyochaguliwa ni pamoja na Accra (Ghana), Enugu (Nigeria), Kigali (Rwanda), Cali (Colombia), Juarez (Mexico), San Juan (United States), Santa Fe (Argentina), Santiago de los Caballeros (Dominican Republic), Santiago na Metropolitan Region (Chile).

Europa miji iliyochaguliwa ni Athens (Greece), Barcelona (Spain), Belgrade (Serbia), London (Great Britain), Lisboa (Portugal), Milan (Italy), Paris (France), Thessaloniki (Greece), Amman (Jordan).  Kaskazini ya Mareica miji ni pamoja na: Boston (United States), Chicago (United States), Dallas (United States), Montreal (Canada), Pittsburgh (United States), St. Louis (United States) and Tulsa (United States). Miji mingine ni Sydney(Australia), Wellington City (New Zealand), Bengaluru (India), Chennai (India), Deyang (China), Huangshi (China), Phnom Penh (Cambodia), Singapore (Singapore), Toyama (Japan)