Arsene Wenger kalipa £16million kwa ajili ya kumsaini Danny Welbeck.

Welbeck, aliambiwa anaweza kuondoka Old Trafford baada ya kushindwa kumvutia Louis van Gaal, mwanzoni United ilikua ni dili la mkopo wenye thamani ya £3m.
Lakini Welbeck,23 alidhamiria kuondoka jumla na kuanza upya sehemu nyingine. United walitaka £18m kabla ya kufikia makubaliano ya £16m na kumpatia Welbeck mkataba wa miaka mitano.

– Loic Remy £8m jumla, Balotteli £16m jumla, Falcao £12m mkopo kwa mwaka, Bony £20m jumla, Chicharito £2.1m kwa mkopo, Negredo £2.5m kwa mkopo.

Tofauti ya Wenger na makocha wengine:
Chelsea wakiwa tayari wana Diego Costa wamemsajili Remy.
United wakiwa tayari wana RVP, Di Maria na Rooney wamemsajili Falcao.
City wana Dzeko, Jovetic, Aguerro.
Sisi tukiwa hatuna straika wa maana na hata huyo tunayemtegemea akiwa atakaa nje kwa nusu msimu tunamnunua Welbeck ambaye ni muhali kufunga bao 15 kwa msimu asaidiane na Sanogo huku akiwa hataki kumtumia Joel Campbell ambaye msimu ujao anaingia mwaka wake wa mwisho was mkataba na atakua huru kuanza mazungumzo ya awali kujiunga na klabu yoyote bure msimu utakaofuata.

14216_308039749368468_1093580717880160367_n

source