APRM Tanzania yaipongeza Thehabari Blog

Katibu Mtendaji APRM Tanzania, Bi. Rehema Twalib

THE AFRICAN PEER REVIEW MECHANISM (APRM)
APRM Tanzania
5th Floor NIC Investment House,
P.O. Box 8315, Dar es Salaam
Telephone: 255 22 2129262/4/5/7
Fax: 255 22 2135029
Email: aprm@aprmtanzania.org
Web: www.aprmtanzania.org

APRM/CRM/2012/105 29 Machi, 2012

Mhariri Mkuu
The Habari.com Blog
DAR ES SALAAM

YAH: KUWASHUKURU KWA USHIRIKIANO/ KURIPOTI UJIO WA TIMU YA WATAALAMU (CRM) CHINI YA MPANGO WA APRM
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Usimamizi la Taifa (NGC) la Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) linayofuraha kuwasilisha kwako na kwa niaba ya timu yako nzima ya watendaji waandamizi, wahariri na waandishi wa habari, salamu zetu za shukrani za dhati kwa ushirikiano tulioupata kutoka chumba chako cha habari.

Itakumbukwa kuwa kati ya Machi 2-23 mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilialika jopo la wataalamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuja kutathmini Ripoti ya Ndani ya Hali ya Utawala Bora iliyokuwa imeandaliwa na APRM Tanzania.

Kama mnavyofahamu, wakiwa hapa nchini wataalamu hao walikutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utawala bora akiwemo Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Sekta Binafsi.

Katika kipindi hiki muhimu na cha kihistoria katika mchakato huu wa APRM na kwa nchi yetu, na hata kabla ya hapo, ofisi yako ilikuwa miongoni mwa nyenzo muhimu katika kufikisha habari kwa wananchi na wadau wa utawala bora kwa ujumla.

Kazi mliyoifanya ni kubwa na yenye manufaa makubwa kwa Taifa letu na itabaki kuwa kielelezo muhimu na cha milele kwa vizazi vijavyo juu ya ushiriki wenu katika kusaidia kuijenga Tanzania imara zaidi.

Wakati tukisubiri ripoti ya wataalamu hao ili nchi yetu ianze kufanyiakazi maoni yao na ya wananchi wa Tanzania, tunawaahidi kuwa ninyi kwa ujumla wenu, mtaendelea kuwa wadau wetu wa karibu katika shughuli mbalimbali za APRM.

Natanguliza shukrani.

Wako
APRM Tanzania

Bi. Rehema Twalib
Katibu Mtendaji