Apollo Wavuna Viungo 23 vya Binadamu Waliojitolea

Apollo-Chennai-swah
KAMA watoa huduma za afya wanaoongoza barani Asia Hospitali za Apollo zimekuwa maarufu na kukubalika kwa mafanikio yake kitabibu na kujitoa kwake katika kuboresha maisha ya watu. Katika hali ambayo hutokea mara chache kati ya wataalamu wa utabibu Apollo waliendesha zoezi la upandikizaji wa viungo kwa kipindi cha siku moja. Matukio yaliyofanyika tarehe 4 Mei 2015 chini ya Hospital kuu ya Apollo Chennai, India ilishuhudia timu ya madaktari ikivuna viungo 23 tofauti tofauti vya mwili kutoka kwa watoaji tofauti watano.

Utofauti wa tukio hili pengine ni kuwa ni mara ya kwanza familia tano zilizofiwa kujitokeza kwa wakati mmoja na kukubali kujitolea viungo vya mwili wa mpendwa wao marehemu aliyefariki punde ili kuokoa maisha ya wengine. Kitendo hiki cha kihistoria kinaonesha Ubinadamu wa familia hizi zilizo katika kipindi kigumu kimeushangaza ulimwengu wa kitabibu na katika mchakato huu kuweka rekodi ya kiasi kikubwa cha viungo kuwahi kuvunwa kwa siku moja.

Timu ya madaktari 100 wenye taaluma mbalimbali ilitumia sehemu 7 za vyumba vya upasuaji kwa wakati mmoja kuvuna viungo 23 na kufanya upandikizaji wa viungo 10 kwa wakati huohuo. Madaktari na wafanyakazi wasaidizi walifanya kazi masaa 12 kusaidia tukio hili la kukumbukwa, iliyo ongeza tena sifa nyingine kwa mafanikio ya Hospitali za Apollo katika kuendesha shughuli nyingi zaidi za upandikizaji viungo duniani.

Katika kupongeza ukarimu wa familia zilizojitolea, hospitali za Apollo ziliandaa sherehe kwa lengo la kuelezea shukrani zao kwa familia hizi. Sherehe ilihudhuriwa na muanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dkt. Reddy, Makamo mwenyekiti, Bi. Preetha Reddy na timu yote ya madaktari ambao walihusika katika kuhakikisha mafanikio ya mchakato huu.

Akihutubia mkutano Dkt. Reddy alisema “Leo, familia hizi zenye nia njema zimesaidia kuwapa nafasi nyingine ya kuishi watu walio katika hatua za mwisho kwa viungo vyao kushindwa kufanya kazi – na kitendo kitawahamasisha watu wengi zaidi kuchangia viungo. Inahitaji dhamira ya ziada kiubinaadamu na kupevuka kwa dhamira ya uwajibikaji wa familia kuzisaidia jamii, hospitali na madaktari kutoa nafasi mpya ya maisha kwa wale wanaohitaji. Uhai wa binadamu haununuliki, na maisha ya mtu yanapoweza kutoa uhai na matumaini kwa wengine wengi wanaohitaji, kwa hakika hakuna cha kulipia!”

Watanzania wengi katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakitafuta huduma za kitabibu zaidi nchini India sababu ya maendeleo na urahisi wa huduma hizi nchini India. Kwa sasa Tanzania zoezi la kujitolea viungo halupo, kuundwa kwa sera na taratibu za mchakato huu katika nchi kutasaidia watu wengi. Nchi kama India wanafaidika kwa kuwepo kwa sera hii inayoruhusu watu kufaidika kwa ukarimu wa wanafamilia wa marehemu kujitolea viungo vya mpendwa wao au marehemu mwenyewe kujitolea.

Hospitali za Apollo zinaongoza duniani kufanya shughuli nyingi na kufanikisha upandikizaji wa viungo duniani na kuwa na matokeo mazuri zaidi kuliko duniani. Ni kitovu kikuu cha rufaa kwa upasuaji usiokuwa na madhara makubwa na kinapokea Idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Dunia nzima ikiwemo Tanzania wakitafuta huduma bora na rahisi za matibabu kwa kutumia muda mfupi pasipo kusubirishwa. Zaidi ya wagonjwa wakigeni 200,000 kutoka zaidi ya nchi 120 wamefanikiwa kutibiwa magonjwa mbalimbali kitaalamu katika hospitali za Apollo.

Hospitali za Apollo hivi karibuni zilipata Tuzo ya dhahabu ‘Golden Peacock’ kutoka taasisi ya wakurugenzi, kwa kushirikiana na kitengo cha sera na uendeshaji, Serikali ya India. Hii ni tuzo ya juu zaidi ya ubora wa biashara katika sekta ya afya, na kuchukuliwa kama kipimo cha kiwango katika tuzo za ubora wa kampuni. Hospitali za Apollo ilipokea tuzo hii kwenye sherehe iliyofana iliyofanyika katika Mkutato wa 25 wa Dunia juu ya ‘Uongozi wa Ubora wa biashara na Ubunifu’ hivi karibuni Dubai.

Kama tu ukarimu uliooneshwa na familia hizi 5, kwa kujitolea viungo vya wapendwa wao, utakuwa tochi kuwaangazia wengine kufwata mfano huu, inamaana kuwa wagonjwa wengi zaidi ambao viungo vyao viko katika hatua za mwisho kushindwa kufanya kazi na wanaohitaji zaidi watafaidika kwa mwanzo mpya wa maisha.

JINSI GANI VIUNGO HIVI VILIFAIDISHA WATU TOFAUTI:
Kutoka kwa marehemu watano waliojitolea, figo 10, pea 3 za macho (jumla ya macho 6), mioyo miwili (2) na maini mitano (5) vilipatikana:
• Maini mitano (5) yalitumika Apollo
• Moyo mmoja (1) ulitumika Apollo na mmoja (1) Fortis
• Figo nne (4) Apollo
• Figo nne (4) zilitumwa KGH, Coimbatore
• Figo moja (1) ilitumwa Hospitali ya Kamakshi
• Figo moja (1) ilitumwa Hospitali ya Global
• Macho sita (6) yalitumwa Sankara Nethralaya