Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wakiendelea kufanya usafi kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani akitoa maelekezo ya kufanya usafi kuzunguka ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile (wa tatu kulia) akielekea eneo la kufanya usafi kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis akishiriki kufanya usafi katika kituo hicho ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli kuwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru 2015 yatumike kwa kufanya usafi nchini kote.
Meneja wa Kituo hicho, Shadrack Mwamaso naye akishiriki kufanya usafi.
Hapa usafi ukiendelea.
Hapa ni kazi usafi ukifanyika.
Ni kama anaongea ‘Ngoja nikazitupe taka taka hizi eneo husika”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis (kushoto), akiwaelekeza jambo wafanyakazi wenzake wakati wakifanya usafi katika kituo hicho.
Hapa ni usafi tu kwa kwenda mbele.
|
Hapa ni bega kwa bega katika kufanya usafi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis akiwa sanjari na wafanyakazi wenzake wakati wa kufanya usafi. |
Wafanyakazi wa kituo hicho wakifanya usafi. Kushoto ni Ali Hussein na Charles Nkwera (kulia)
Takataka zilipelekwa eneo husika.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYAKAZI wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wameungana na watanzania nchini kote kufanya ufasi ikiwa ni utekelezsaji wa agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli la kuitumia siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania 2015 kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Brown Francis alisema wamejisikia furaha kubwa kutekeleza agizo la Rais kwa kufanya usafi katika eneo lao la kazi.
“Tulijipanga na wafanyakazi wenzangu katika kutekeleza jambo ili ambapo ni muhimu kwa taifa letu la kufanya usafi wa mazingira na litakuwa ni endelevu” alisema Francis.
Francis alisema ni muhimu kwa kila mtanzania kujenga tabia ya kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo yao badala ya kusubiri kuhimizwa na viongozi.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Zanlink Zanzibar wakiitikia wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Wakishiriki katika zoezi la Usafi wa Mazingira katika sehemu yao ya Kazi kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru.
Mfanyakazi wa Zanlink Zanzibar akishiriki katika Zoezi la Usafi kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara imeadhimishwa Kitaifa kwa Usafi wa mazingira.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe.Ussi Salum Pondeza AMJAD akishirikiana Wananchi wa Jimbo lake kutekeleza Wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufu wa Hapa Kazi Tu. kwa kufanya usafi katika maeneo ya Jimbo lao.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakishiriki katika Usafi wa Mazingira ya Jimbo Lao.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifanya Usafi katika maeneo ya Jimbo lao wakijumuika na Mbunge wao Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD katika kuitikia Wito wa Hapa Kazi Tu, kuadhimisha Miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika.
Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imesherekea sherehe za Uhuru wa Tanganyika, Disemba 9 kwa kufanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach kama jinsi alivyoagiza rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuagiza kuwa siku ya Uhuru itumike kufanya usafi kutokana na kushamiri kwa uchafu katika mazingira yanayotuzunguka.
Kwa kufata agizo hilo la Dk. Magufuli, MeTL Group kwa kujumuisha viongozi wa kampuni na wafanyakazi wake imefanya usafi kwa pamoja katika ufukwe wa Coco Beach ili kusafisha eneo hilo ambalo linatumiwa na watu wa aina mbalimbali kwenda kujipumzisha pamoja ndugu na familia siku za mapumziko.
Hizi ni baadhi ya picha wakati wafanyakazi wa MeTL Group wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach;
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer (kulia) akiongoza na Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Kijumbe kuelekea kwenye eneo la usafi mara baada ya kuwasili kwenye fukwe za Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote Dec 9, 2015.
Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL Group wakiwasili kwenye fukwe za Coco Beach kushiriki zoezi la usafi.
#HapaKaziTu.…….Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer (kulia) akisaidiana na Kiongozi Mahusiano ya Kazi wa MeTL Group, Subrina Gulamali Bhatti kubeba moja ya gogo lililokuwa linazagaa kwenye fukwe hizo.
Wafanyakazi wa makampuni ya MeTL Group wakiendelea na zoezi la usafi katika fukwe za Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote Dec 9, 2015.
Zoezi la kukusanya takataka na kuchoma mifuko ya nailoni iliyokuwa imezagaa kwenye fukwe za Coco Beach likiendelea.
Wengine wakiendelea kufyeka vichaka vya majani katika fukwe za Coco Beach.
Zoezi likiendelea.
Takataka zikiendelea kukusanywa na kuchomwa moto.
Takataka zikikusanywa kwenye viroba.
Zoezi likiendelea kwa ushirikiano wa hali ya juu.
#HapaKaziTu ndio maneno waliyokuwa wakisema wafanyakazi wa MeTL Group wakiendelea na zoezi la kusafisha fukwe za Coco Beach jijini Dar.
Baadhi ya wafanyakazi wa MeTL Group katika picha ya pamoja.
Picha za kumbukumbu baada ya kazi zilipigwa.
Mkuu kitengo cha Rasimali watu anayeshughulikia wafanyakazi wa ndani (Local) kampuni ya MeTL Group, Masuma Mushtak (waliosimama wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Makao Makuu ya Ofisi za MeTL Group.
|
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Moshi,Emanuel Kishosha akishiriki na wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya uwanja wa michezo wa King George. |
|
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wa matawi ya Mandela na Mawenzi Mjini Moshi, Kilimanjaro wakishiriki zoezi la usafi Siku ya 9 Desemba. |
|
Wafanyakazi wa NMB wakihakikisha hakuna uchafu unasalia katika uwanja wa michezo wa King George. |
|
Kazi ya ukusanyaji taka ikiendelea. |
|
Kila mfanyakazi alishiriki zoezi la usafi bila ya kuchoka. |
|
Meneja wa NMB,Emanuel Kishosha akisukuma tololi kuzoa taka. |
|
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini (kushoto) mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika uwanja wa michezo wa King George . |
|
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha akiwashukuru wafanyakazi wenzake wa benki hiyo kwa kujitokeza katika zoezi la kufanya usafi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755659929) |
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakishusha vifaa vya kufanyia usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakishusha vifaa vya kufanyia usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakigawana nyenzo za kufanyia usafi kabla ya kuanza usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Thomas (katikati) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kufafanua juu ya zoezi la usafi lililofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika Soko la Temeke Stereo pamoja na kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi. |
|
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa pili kulia) akikabidhi baadhi ya vifaa vya usafi kwa Ofisa Masoko Manispaa ya Temeke, Tito Nombo (mwenye shati jeupe) kabla ya kuanza zoezi la kusafisha maeneo mbalimbali ya soko la Temeke Stereo la jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa TTCL na maofisa wa soko la Temeke wakishuhudia zoezi hilo. |
|
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakifanya usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakifanya usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Thomas (kulia) akifanya usafi katika Soko la Temeke Stereo leo asubuhi jijini Dar es Salaam. |
|
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakifanya usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakifanya usafi katika soko la Temeke Stereo jijini Dar es Salaam leo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliyeamuru Siku ya Maadhimisho ya 9 Desemba itumike kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekua ukiibuka mara kwa mara na kupoteza maisha ya wananchi. |
|
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaidiana na wafanyakazi wenzake kufanya usafi katika Soko la Temeke Stereo leo asubuhi jijini Dar es Salaam. |
|
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaidiana na wafanyakazi wenzake kufanya usafi katika Soko la Temeke Stereo leo asubuhi jijini Dar es Salaam. |
|
Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akisaidiana na wafanyakazi wenzake kufanya usafi katika Soko la Temeke Stereo leo asubuhi jijini Dar es Salaam. |