Ancelotti Avizia Kibarua Cha Van Gaal.

2102342_heroa
Carlo Ancelloti mwenye umri wa miaka 56 ambaye alihusishwa kuhamia Old Trafford mwaka 2014 bada ya David Moyes Kufukuzwa, kabla ya Louis van Gaal kupata nafasi, sasa amekiri kutaka kuinoa klabu hiyo.

Ancelotti amekiri kuwa angependa kurudi Ligi Kuu ya Uingereza na inaelezwa kuwa pendekezo lake ni kukinoa kikosi cha Manchester United kilichipo chini ya Luis Van Gaal raia wa Uhoranzi.

Kocha huyo aliyekuwa akikinoa kikosi cha Real Madrid Kabla kibarua chake kuota nyasi mwezi Mei mwaka huu amesema anataka kurudi tena kwa kasi ili kuilejeshea Man United makali yake.

“Bila shaka, kwa kila meneja, wangependa kuifundisha Klabu ya Manchester United kutokana na umaarufu wa klabu hiyo.”

“sijutii kuondoka Real, kwa sababu kila mtu anajua makubwa na mazuri niliyoyafanya katika klabu ile.

“Nilipokwenda PSG,hawakuwa na tamaduni kama ilivyokuwa kwa Madridi au Millani lakini kama watafanya juhudi zaidi basi wataendelea kuwa klabu kubwa na imara duniani kwa siku za mbele kama zilivyo kuwa Barcelona na Mdridi”

Ancelotti, ambaye alishinda taji la ligi, kombe la FA na Ngao ya Jamii wakati akiwa anaitumikia klabu ya Chelsea bado anandoto ya kurudi tena Uingereza msimu ujao kwenye ligi ya Ushindani na inayopendwa zaidi Duniani.