Aliyeipa Ubingwa wa AFCON Nigeria Afunguka..!

Wachezaji wa Nigeria wakishangilia ubingwa wa AFCON

Muuaji wa Buki Nabe katika fainali za AFCON, Sunday Mba

MFUNGAJI wa bao pekee la ushindi la Nigeria, Sunday Mba aliyeiwezesha Super Eagles kuilaza 1-0 Burkina Faso na kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika, amesema ‘Ndoto zimekuwa kweli.’

Mba aliiwezesha Super Eagles kuandika historia ya kutwaa taji la tatu la Mataifa ya Afrika, na la kwanza tangu mwaka 1994, kwa kufunga bao baab kubwa dakika tano kabla ya mapumziko.

Nigeria ilitawala mchezo wa jana na Burkina Faso walikuwa wana wakati mgumu uwanjani, wakichea fainali yao ya kwanza kabisa ya michuano hiyo. Matchwinner: Sunday Mba’s goal gifted Nigeria victory over Burkina Faso Sunday Mba akishangilia bao lake jana

Mba, ambaye anachezea timu ya Ligi Kuu ya Nigeria, Warri Wolves, anaamini matokeo hayo yatasaidia kumuinua kisoka baada ya mashindano haya.

‘Nina furaha ile mbaya, ndoto zimekuwa kweli. Sijui niseme nini. ‘Kweli tulipigana haswa na akili yetu ilikuwa kwenye mechi ya leo (jana) na nina furaha sana,”alisema jana Mba. Champions: Nigeria are the 2013 African Cup of Nations champions Mabingwa Nigeria wakishangilia.

‘Itasaidia sana kuniinua kisoka. Hii ni mara yangu ya kwanza na nina furaha sana. ‘Tulitoa kila tulichokuwa nacho.’ Hiyo ilikuwa fainali ya kwanza kwa Nigeria tangu mwaka 2000 na wameendeleza rekodi ya kucheza mechi 12 bila kufungwa.

Ushindi huo unamaanisha kocha Stephen Keshi anakuwa kocha wa pili tu kutwaa taji hilo kwanza kama mchezaji na baadaye kocha, akifuata nyayo za Mmisiri, Mahmoud Al Gohari.