WANAMGAMBO wa Al-Shabab nchini Somalia wanasema kuwa watamuua jasusi wa Ufaransa Denis Allex, ambaye Ufaransa ilisema kuwa alikuwa tayari ameuawa wakati jaribio la kumuokoa lilipotibuka.
Walisema kuwa Ufaransa inapaswa kulaumiwa ikiwa atauawa. Na pia inapaswa kulaumiwa kwa mauaji ya makomando wengine wawili waliouawa Ijumaa katika msako uliofanywa mjini Bulo Marer.
Maafisa nchini Ufaransa wanasema kuwa waliamini bwana Allex alikuwa ameuawa na mateka wake wakati wa jaribio la kumuokoa ingawa al-Shabab wanasema hakuwepo hapo wakati huo.
Al-Shabab imetuma picha ya mwili wa komando mmoja, aliyeuawa lakinin sio wa Allex, jina la kikazi la jasusi huyo ambaye amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miaka mitatu.
Katika ujumbe wao kupitia Twitter, al-Shabab walisema ufaransa ndiyo imesababisha kuuawa kwa Alex kwa sababu ya njama yao ya kutaka kumuokoa.
Waziri wa ulinzi aliambia idhaa ya redio ya ufaransa, kuwa anaamiini Alex ameuawa tayari, na kuituhumu Al Shabaab kwa kuchzea hisiasa za watu.
Ufaransa inasema kwamba makombando wa Ufaransa waliwaua wanamgambo 17 Ijumaa. Walioshuhudia makabiuliano hayo wanasema kuwa raia kadhaa pia walifariki kwenye makabiliano hayo.
Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, alisema Ufaransa ilichukua hatua kwa sababu ya kile ilichosema ni madai ya kupuuzi yaliyokuwa yanatolewa na Al-Shabab.
-BBC