Ajali Mbaya Yatokea Mbeya Yauwa 10 na Kujeruhi 25

Gari ambalo alikuwemo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Mwanjelwa likiwa limeteketea kwa moto baada ya ajali.


Baadhi ya magari yaliohusika katika ajali hiyo yakiwa yameharibika vibaya


Lori la mafuta lililosababisha ajali hiyo likiendelea kuteketea kwa moto huku wananchi wakishuhudia muda mfupi baada ya ajali hiyo.


Mbunge Mary Mwanjelwa akiwa amelazwa hospitalini baada ya kuokolewa kwenye ajali hiyo.

WATU kumi wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Mwanjelwa baada ya lori la mafuta kushindwa kushika breki na kuyagonga magari mengine matatu katika mtelemko wa Mlima wa Iwambi eneo la Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Katika ajali hiyoiliyotokea majira ya saa nane mchana, Mbunge Mwanjelwa alinusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria, kugongwa na kuteketea kwa moto kabisa na kusababisha kifo cha Katibu wake. Mbunge huyo kwa sasa amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi pamoja na majeruhi wengine.

Baadhi ya watu waliioshuhudia ajali hiyo, walisema lori hilo la mafuta lilishindwa kushika breki na kuanza kutelemka kwa kasi katika mlima huo, ambapo liliyagonga magari matatu ikiwamo gari dogo la abiria (Hiace) yenye namba za usajili T 587 AHT na kuleta madhara zaidi.

Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi alisema Mbunge Mwanjelwa analalamika zaidi maumivu katika sehemu ya mgongoni na miguu sawa na dereva wake ambaye naye analalamikia miguu na amepasuka sehemu ya kichwani. Majeruhi wengine wengi wamekatika miguu kutokana na kitendo cha lori hilo kugonga gari aina ya hiace ubavuni kabla ya kuanguka.

Picha zote na Habari kwa Hisani ya Mbeya Yetu Blog.