Airtel yazindua internet ya kasi na bora aina ya 3.75G

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya 3.75G uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel watapata internet


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sam Elangallor akionesha jinsi huduma ya 3.75 inavyoweza kutoa huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwawezesha wateja wa Airtel kufanya video call wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75 iliyofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, kulia ni Mkurungezi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na kushoto ni

Na Joachim Mushi

KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua huduma ya mtandao wa internet yenye kasi na ubora itakayowawezesha wateja wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet kufanya shughuli mbalimbali za kutuma na kupokea data anuai kulingana na matumizi ya mteja.

Huduma hiyo ya mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa, iliyozinduliwa nchini leo itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi bila kujali eneo ambalo mtumiaji yupo kwa kutumia simu, huku wakiwa na uwezo wa kumwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na hata kuperuzi kwenye tovuti.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel, Sam Elangalloor amesema huduma hiyo ya 3.75G yenye ubora na kasi ya hali ya juu itawawezesha wateja wake katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano (multimedia), kufungua tovuti anuai, kufanya mazungumzo ya simu kwa njia ya video, kuangalia televisheni na kupata miziki kwenye tovuti kwa kutumia simu.

Mkurugenzi wa Airtel, Sam Elangallor akiinua modem na kumkabidhi Mwandishi wa habari kutoka TBC, Jane John aliyejishindia modem wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.


“Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya juu na kasi zaidi,” alisema Elangalloor.

Alisema Airtel inafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao
kwa kuzingatia mahitaji ya teknolojia hiyo duniani hasa kwa huduma za kimtandao kupitia simu ya mkononi.

“Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co. Telecommunications zinaonesha mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba Bara la Afrika ni moja kati ya soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi likiendelea kukua na kufikia kutoa huduma za internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking) na biashara kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce).” Alisema.

Aidha alisema kampuni ya Airtel itaendelea na mikakati ya kuwaletea wateja internet zenye kasi zaidi kama ilivyo kwa 3.75G ambayo ni sambamba na malengo ya kuendea mtandao ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara la Afrika.

“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini tutaweza kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani
na nje ya ya jamii zetu,” alisema Elangalloor.

Akifafanua mara baada ya mteja kuunganishwa na teknologia ya 3.75G, simu yake
itaonesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA; huku ikitegemeana na aina ya simu anayotumia- lakini kasi ya kuunganishwa itakuwa na ubora zaidi.

Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watumiaji