Airtel yazidi mawasiliano vijijini, yaingia Ruvuma


Nembo ya kampuni ya Airtel.

*Yazindua mnara wa mawasiliano maeneo ya Mganizi

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa mtandao mpana wa mawasiliano, leo imetimiza ahadi yake ya kuleta mawasiliano nafuu na yenye kuwafikia watanzania wengi zaidi kwa kuzindua huduma ya mawasiliano katika Mkoa wa Ruvuma
Akitoa maoni yake juu ya huduma ya mawasiliano, Mkurungezi wa mauzo na Biashara, Cheikh Sarr, Amesema Airtel imejizatiti na kutoa kipaombele kupeleka mawasiliano katika maeneo ya vijijini ili kuwezesha kuendeleza shughul muhimu za kiuchumi kama kilimo, uvuvi , madini na biashara kwa ujumla”
Sarr alisema “Airtel inadhamiria kwa mwenzi huu tu kuzindua mawasiliano yake katika maeno yapatayo 50 nchi zima, uwepo wetu Mganizi na maeneo jirani, kwa hakiki kutaleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiumchumi kwa wakazi , wageni na wakazi wa maeneo jirani . Tunategemea kuweza kwafikia wananchi wapatao takribani 3000.
Kuwaunganisha watu wa Ruvuma wakati huu ambapo mahitaji ya mwasilano ni makubwa, kunadhihirisha dhamira yetu ya kuwa mbele zaidi na tofauti kwa kila tunalofanya. Tunafurahi kuwa wakwanza na kuwaahidi watanzania kuwa tutaendeleza kupanua huduma zetu katika miji na vijiji mbalimbali vya Tanzania ambavyo mtandao wowote bado haujafika.
Akitoa maoni yake juu ya uzinduzi huu wa mawasiliano, Meneja wa Mkoa Frederick Mwakitwange alisema,” Airtel imedhamiria kuendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa wakazi wa Ruvuma huku ikiendeleza kuongeza mtandao wake kwenye maeno mengi ya mkoa huu na kuwapati wateja wake uzoefu tofauti na wa kipekee katika huduma hizi za simu ambazo zimewafikia wananchi wa vijiji na miji mingine Tanzania .
Kuwepo kwa mtando wa mawasiliano Ruvuma kutainua shughuli za uchumi za kilimo na kuwezesha sera ya nchi ya kilimo kwanza kufikia malengo yaliyokusudiwa,”alisema Frederick.
Kwa kuwepo kwa Airtel sasa hivi kutawawezesha watu kuweza kupiga na kupokea simu, na ujumbe mfupi (sms), kutumia huduma nafuu ya internet na pia kuweza kutuma na kupokea fedha kupitia Airtel money na kuondoa usumbufu uliokuwepo awali wa kutopata taarifa na huduma muhimu. leo hii wakazi Mgazini wataweza kupiga na kupokea simu wakiwa majumbani na sehemu zao za biashara.