Airtel yasaidia vitabu Secondari ya Kondoa

Ofisa mauzo wa Airtel Kanda ya Kati, Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya taaluma, Ibrahim Juma Mwesi Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Itaswi katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma, Hurui, Gubali na Itaswi, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu Mkuu wa Shule ya Sekendari Gubali.

Ofisa Mauzo wa Airtel Kanda ya Kati, Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya taaluma, Leonard Cyprian Ngotta Mwalimu wa taaluma Shule ya Sekondari Hurui katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma, Gubali, Itaswi na Hurui, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu Mkuu wa Shule ya Sekendari Gubali.

AIRTEL yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa- Dodoma Chini ya mpango wake wa shule yetu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari zilizoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo na katika kutoa huduma kwa jamii.

Makabithiano hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali na shule ya sekondari zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Sekondari ya Goma, Gubali, Itaswi na Hurui, zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa kila shule.

Akizungumza katika hafla ya makabithiano Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Kanda ya Kati, Hillary Tarimo alisema” Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule za sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule zitakazokabithiwa.

Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika
kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu
ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza
Tarimo.

Naye Makamu mkuu wa shule ya sekondari Galibu, Kessy Musilenga
alisema” nachukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kutufikia na kutoa
msaada wa vitabu kwa shule zetu na kupunguza changamoto zilizokuwepo katika shule hizi, tunayofuraha kwa shule yetu na wenzetu wa shule za jirani zilizopo wilayani kondoa kupata nyenzo muhimu ambazo zitainua kiwango cha elimu kwa wakazi na wanafunzi wa wilayani”

Tunawaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo
vizuri kwa wanafunzi, Tunaamini jamii ikipata elimu bora maendeleo ya
shughuli mbalimbali za uchumi yatafanyika kwa ufanisi zaidi na kuleta
mafanikio makubwa kwa jamii. Aliongeza Kessy.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, siku chache zilizopita Airtel
ilitoa msaada wa computer 20 na vitabu vyenye thamani ya million 10
kwa chuo kikuu cha Dodoma – UDOM hii ni katika kurudisha faida
inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.