MASHINDANO ya vijana chini ya miaka 17 yaliyopewa jina la ‘Airtel Rising Star’ yataaza kutimua vumbi leo, ambapo Mkoa wa Dar es Salaam utatumika kupitia viwanja vyake vya Airwing, Makongo na Twalipo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel, Jackson Mbando alisema kuwa kampuni yao kwa kushirikiana na timu ya Manchester, wameamua kufanya mashindano hayo ili waweze kupata wachezaji watakaoenda katika kituo cha timu hiyo.
Mbando alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya timu za Sekondari 24 kutoka katika mikoa ya Dar es Salaa, Morogoro, Iringa na Mwanza.
Alisema michezo ngazi ya mkoa imepangwa kumalizika mwezi huu na kila mkoa shiriki utamtangaza bingwa wake tayari kwa fainali za Airtel Rising Stars zitakazofanyika Dar es Salaam.
Mbando alisema hatua zitakazofuata baada ya timu 24 itakuwa timu tanane na baadae kutafuta wachezaji 20 kwa kila mkoa na baadae kuchujwa na kubaki sita ambao wataondoka nchini kwenda Manchester.
Mbando alisema katika michuano ya hatua ya fainali licha ya kuwepo makocha wa hapa nchini, makocha kutoka Manchester United watakuwepo kuhakikisha wanapatikana vijana watakaowakilisha Tanzania.
Fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zitafuatiwa na kliniki ya soka kimataifa kwa nchi zinazoongea kiingireza ambayo pia yatafanyika Tanzania na kusimamiwa na makocha mahiri kutoka Manchestaer United ya England.
Mbando alisema Tanzania itawasikilishwa na wachezaji sita nyota wakaoteuliwa wakati wa fainali hizo.
Baadhi ya timu zinazoshiriki ni Makongo Sekondari, Twiga Sekondari, Mpigimagohe Sekondari, Goba Sekondari.
Nyingine ni Jitegemee, Mbande, Kibugumo, na Timeke, wakati nyingine ni Azania, Kinyerezi, Misitu, Sua, Mwembesongo, Kibanda , Morogoro, Mwanza, Busweru, na Lugalo Sekondari.