Ahmed Musa wa Leicester City Apiga Mbili mwenyewe Mbele ya Barcelona

barca

Mchezaji ghali zaidi kununuliwa na Leicester City Ahmed Musa, aliyenunuliwa pauni milioni 16 na kuvunja rekodi ya klabu hiyo, amewafungia mabao yote mawili katika mechi ambayo wamefungwa 4-2 na Barcelona katika michuano ya Kombe la Kimataifa la Klabu.

Munir alifungua ukurasa wa mabao kupitia pasi iliyotoka kwa Lionel Messi kabla ya nyota huyo wa Argentina muda mfupi baadaye kumuandalia pasi safi Luis Suarez aliyeongoeza la pili katika mchezo huo uliochezewa uwanja wa Friends Arena mjini Stockholm, Sweden. Munir aliongeza la tatu, kabla ya Musa kukomboa bao moja.

Musa alifanikiwa kukomboa la pili lakini nguvu mpya wa Barca Rafa Mujica, mwenye umri wa miaka 17 pekee, akaifungua Barcelona la nne dakika za mwisho mwisho.

Mshambuliaji Jamie Vardy, aliyeongeza muda wa mkataba wake kwa miaka minne mwezi Juni, na Riyad Mahrez, ambaye amehusishwa na kuhamia Arsenal, wote walianza kwenye kikosi cha Leicester
kitakachokabiliana na Manchester United katika mechi ya Ngao ya Jamii uwanjani Wembley siku ya Jumapili.

Upande wa Barca, kando na Messi na Suarez, kulikuwa na nyota wengine kama vile Javier Mascherano na Sergio Busquets.Leicester wataanza kutetea taji lao la Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City ugenini mnamo tarehe 13 Agosti.

Nayo Bayern Munich imechapwa bao moja kwa bila na Real Madrid huku AC Milan ikilala kwa bao 1 kwa 3 dhidi ya Chelsea