Bi. Risper Muthamia amesema kuwa Filamu zote zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni na mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) zinaweza kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo zilitengenezwa na kurushwa hewani au kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha kati ya May 1, 2011 hadi April 30, 2012.
Aidha amefafanua kuwa Filamu au vipindi vitakavyoshiriki katika tuzo hizo viwe ni katika lugha ama ya Kiingereza, Hausa (Nigeria), Swahili au Yoruba na kusisitiza kuwa hakuna Lugha nyingine itakayokubalika.
Ameongeza kuwa Filamu na Sinema zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni zinapaswa kuwa na urefu wa kati ya Dakika 60 mpaka 90 wakati Mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) ni kwa muda wa dakika 30 mpaka 60. Wasanii wamekumbushwa kuwa ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo wanapaswa kuwasilisha nakala 6 za DVD za filamu zao.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza katika semina fupi ya wadau wa tasnia ya Filamu nchini pamoja na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa wasanii watakaopelekea kazi zao wahakikishe kuwa sio za kuiga na zina hati halali ya kusajiliwa na COSOTA.
Msanii wa filamu nchini almaarufu kama Mtitu akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo AMVCA zilizoanishwa na Africa Magic kwa kushirikiana na Multichoice kwa ajili ya kutambua mchango wa wasanii wa bara la Afrika kwa lengo la kukuza sekta ya filamu Kimataifa.
Wasanii wa filamu wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Tanzania na Afrika kwa Ujumla aliyefariki dunia ghafla Marehemu Steven Kanumba.
Msanii wa filamu Cloud naye akichangia mawazo yake wakati wa semina hiyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akiwasisitiza wasanii na watengenezaji wa filamu kuhakikisha zinakuwa na maudhui ya Kiafrika na ubora unaokubalika.
Bw. Mwakifamba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda filamu za nyumbani na kushiriki katika kuzipigia kura pindi zinapokuwa katika mashindano ya aina mbalimbali kama itakavyokuwa katika Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA).
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini waliohudhuria semina fupi iliyohusiana na Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA). Kutoka kushoto ni Msanii Sajuki akiwa amembatana na mkewe na msanii nguli Dk. Cheni.
Mchekeshaji na Msanii wa Filamu Steven Nyerere akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo hizo.
Meneja Masoko wa Mutichoice Tannzania Bi. Furaha Samalu sambamba na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Barbara Kambogi (wa kwanza kulia).
Msanii nguli katika sanaa ya maigizo na filamu hapa nchini almaarufu kama Bi. Mwenda.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Bw. Jai (wa pili kushoto) ambao ni wasambazaji wa filamu nchini akizungumza na maafisa wa kampuni ya Multichoice.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na msanii wa Filamu nchini maarufu kama Cloud.