Mbele ya hakimu, Devota Msofe wa mahakama ya Wilaya Arusha, mwendesha mashtaka wa serikali, Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao, mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30) iliomjeruhi vibaya.
Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani.
Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka, na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo, baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.
Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016, upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa
ikiwemo hati ya polisi(PF3), hati ya daktari pamoja na picha za jeraha. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Februari 6, mwaka huu, saa tatu asubuhi.
Aidha katika hatua nyingine, shahidi namba moja wa kesi hiyo, Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.
Alisema ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio.