Timu ya AFC imeapata kuisambaratisha timu ya JKT Rwankome katika mchezo wa mwendelezo Ligi Daraja la Pili Ngazi ya Taifa (SDL), Utakaochezwa mwishoni mwa wiki hapa jijini Arusha Katika dimba la Sheikh Amri Abeid.
AFC yenye makazi yake jijini Arusha haijafanikiwa kupata pointi hata moja tangu kuanza kwa Ligi hiyo , kwani katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pamba walichezea kichapo cha bao 3-0 kisha mwishoni mwa wiki iliyopita wakilala kwa bao 2-0 dhidi ya Alliance FC ya Jijini Mwanza.
Hata hivyo AFC imekuwa katika hali isiyolidhisha hasa katika michezo ya awali ikisemekana kufanyiwa hujuma na baadhi ya vingozi wa chama cha Soka Mkoni hapa wakishirikiana na wachezaji wachache.
AFC katika mchezo wa kwanza dhidi ya Pamba wakiwa mkoani Mwanza walijikuta wakiingia uwanjani huku katika benchi la akiba Akibaki mchezaji mmoja pekee.
Katibu mkuu wa AFC Salim Kombo alisema kuwa tayari matatizo hayo yameshatatuliwa na kwa sasa wanaanza kuhesabu pointi katika mchezo wa jumamosi dhidi ya JKT Rwankome ili kufanikisha lengo la kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
AFC inajumla ya kikosi cha wachezaji 22 huku wawili wakiwa masomoni ambao ni Humphrey Willium akiwa Chuo cha DIT,na Julius Mwajebele akiwa SUA Mkoani Morogoro.
Sambamba na hilo Katibu Msaidizi wa AFC Charles Mwaimu aliongeza kuwa kuna wachezaji sita wa kikosi hicho wanaonekana kurubuniwa ili wasiichezee AFC ili hali wanamikataba.
“Wachezaji tunaowengi ila wanarubuniwa mfano Aldina Hashim, ,Madaga Luke, Gibson Chuma, Steven Mwakalinga, Samson Mwaluka, na Mohamed Juma” Alisema Mwaimu.
AFC katika SDL imepangwa kundi B ikwa pamoja na Alliance FC ya Mwanza, Madini FCya Arusha, Bulyanhulu FC ya Shinyanga, JKT Rwankome ya Mara , na Pamba ya Mwanza