Abiria wa basi la ABS Express wanusurika kufa

Basi la ABS Express lililoacha njia likitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa

Abiria wa Basi la ABS Express waliokuwa wakisafiri kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Iringa juzi walinusurika kufa (Agosti,17) baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuingia porini. Ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa gari hiyo akiwa katika juhudi za kumkwepa mwendesha baiskeli aliye katisha

Basi la ABS Express likionekana kufunuka mbele baada ya kuchimba chini

Abiria wa Basi la ABS Express waliokuwa wakisafiri kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Iringa juzi walinusurika kufa (Agosti,17) baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuingia porini. Ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa gari hiyo akiwa katika juhudi za kumkwepa mwendesha baiskeli aliye katisha barabarani ghafla. Basi hilo lenye namba za usajili T 180 AUJ lilipoteza uelekeo na kuacha njia lilipokuwa likikaribia kuingia vijiji vya mwanzoni unapoingia mkoani Iringa kutokea mkoani Dar es Salaam. Lilishindwa kuendelea na safari baada ya kuchomoka tairi moja.