Abiria Kwenye Daladala Wanusurika Kifo Tabata, Dar

Daladala aina ya Tata lenye namba za usajili T724BAH linalofanya safari zake kati ya Tabata Segerea na Kivukoni jijini Dar es Salaam, likiwa limegota mtaroni pembezoni mwa barabara ya Mandela eneo la Tabata Dampo baada ya kushindwa kupandisha kwenye muinuko na kuanza kurudi nyuma.

Baadhi ya abiria walionusurika na wapitanjia wakiangalia ajali hiyo muda mfupi baada ya kutokea.

Baadhi ya abiria walionusurika na wapitanjia wakiangalia ajali hiyo muda mfupi baada ya kutokea.

Baadhi ya abiria walionusurika wakiwa pembeni na kuangalia ajali hiyo muda mfupi baada ya kutokea.

Baadhi ya abiria walionusurika wakiwa pembeni na kuangalia ajali hiyo muda mfupi baada ya kutokea.

Eneo la mwinuko ambalo daladala hiyo ilishindwa kupanda kabla ya kuanza kuporomoka.

Na dev.kisakuzi.com, Dar

ABIRIA wa daladala aina ya Tata linalofanya safari zake kati ya Tabata Segerea na Kivukoni jijini Dar es Salaam jana walinusurika kifo baada ya gari hilo kushindwa kupandisha muinuko na kuanza kurudi nyuma ghafla. Tukio hilo lilitokea eneo la Tabata Dampo, ambapo daladala hilo lililokuwa limekodishwa na abiria likitokea Tabata Segerea kushindwa kupanda muinuko wa Dampo kuelekea Gereji na kuanza kurudi nyuma kuelekea barabara ya Mandela kabla ya magurudumu ya mbele kukwama baada ya kuingia mtaroni.

Mashuhuda wa ajali hiyo walisema dereva alikuwa akipandisha mwinuko huo na alipofika katika gia namba moja ilishindwa na kujaribu kuweka namba mbili lakini ilikataa na gari kuanza kurudi nyuma hadi lilipofika pembezoni mwa mtaro wa barabara ya Mandela na kuingia tairi za mbele.

Hata hivyo hakuna abiria aliyejeruhiwa katika ajali hiyo zaidi ya daladala lenyewe kuharibika mfumo wa magurudumu ya mbele baada ya kuingia mtaroni. dev.kisakuzi.com ilishuhudia baadhi ya abiria wakiwa katika makundi wakipeana pole eneo hilo baada ya kunusurika huku askari wa kikosi cha usalama barabarani wakianza kupima ajali hiyo.