Na Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ametangaza majina ya viongozi wanaounda timu ya Sekretarieti ya chama hicho, baada ya uteuzi huo kuidhinishwa na kikao cha hii imetangazwa aleo mjini Dodoma, na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete baada ya uteuzi wake kuidhinishwa na Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichokutana kwa mara ya kwanza mjini Dodoma.
Walioteuliwa katika Sekretarieti hiyo ni Abdulrahman Kinana atakayekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Mwigulu Nchemba atakaeshika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara na Asha-Rose Migiro anayekuwa kuwa kiongozi wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho.
Viongozi wengine wa Sekretarieti ni pamoja na Nape Nnauye anayeendelea na nafasi yake ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na Zakia Meghji atakaye simamia masuala ya Uchumi na Fedha wa chama hicho, huku upande wa Zanzibar Vuai Ali Vuai anashika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.
Kutangazwa kwa safu hiyo ya viongozi kunakamilisha sura ya CCM mpya kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ambao Mwenyekiti wa Chama hicho amewaahidi wajumbwa wa Mkutano Mkuu uliomalizika jana mjini Dodoma kuwa lazima chama hicho kitarudi madarakani kwa kishindo tena.